Mathayo 15:7-9
Mathayo 15:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu: ‘Mungu asema: Watu hawa huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami. Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.’”
Shirikisha
Soma Mathayo 15Mathayo 15:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.
Shirikisha
Soma Mathayo 15