Mathayo 1:21-23
Mathayo 1:21-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Atajifungua mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu, kwa kuwa yeye ndiye atakayewaokoa watu wake katika dhambi zao.” Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii: “Bikira atachukua mimba, atamzaa mtoto wa kiume, nao watampa jina Emanueli” (maana yake, “Mungu yuko nasi”).
Mathayo 1:21-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao. Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Mathayo 1:21-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Mathayo 1:21-23 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Naye atamzaa mwana, nawe utamwita jina Yesu, kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.” Haya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilonena kupitia nabii, aliposema: “Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita jina Imanueli” (maana yake, “Mungu pamoja nasi”).