Mathayo 1:12-17
Mathayo 1:12-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya Wayahudi kupelekwa uhamishoni Babuloni, Yekonia alimzaa Shealtieli, Shealtieli alimzaa Zerubabeli, Zerubabeli alimzaa Abiudi, Abiudi alimzaa Eliakimu, Eliakimu alimzaa Azori, Azori alimzaa Zadoki, Zadoki alimzaa Akimu, Akimu alimzaa Eliudi, Eliudi alimzaa Eleazari, Eleazari alimzaa Mathani, Mathani alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaa Yosefu, mumewe Maria mama yake Yesu aitwaye Kristo. Basi, kulikuwa na vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpaka Wayahudi walipochukuliwa mateka Babuloni, na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwa mateka mpaka wakati wa Kristo.
Mathayo 1:12-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli; Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori; Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi; Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo. Basi vizazi vyote tangu Abrahamu hadi Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hadi ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hadi Kristo ni vizazi kumi na vinne.
Mathayo 1:12-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli; Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori; Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi; Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo. Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vinne.
Mathayo 1:12-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baada ya uhamisho wa Babeli: Yekonia alimzaa Shealtieli, Shealtieli akamzaa Zerubabeli, Zerubabeli akamzaa Abihudi, Abihudi akamzaa Eliakimu, Eliakimu akamzaa Azori, Azori akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Akimu, Akimu akamzaa Eliudi, Eliudi akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Matani, Matani akamzaa Yakobo, naye Yakobo akamzaa Yusufu, aliyekuwa mumewe Mariamu, mama yake Yesu, aitwaye Kristo. Hivyo, kulikuwa na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu hadi Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho wa Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho wa Babeli hadi Kristo.