Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 1:1-17

Mathayo 1:1-17 Biblia Habari Njema (BHN)

Yesu Kristo alikuwa wa ukoo wa Daudi, wa ukoo wa Abrahamu. Hii ndiyo orodha ya ukoo wake: Abrahamu alimzaa Isaka, Isaka alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaa Yuda na ndugu zake, Yuda alimzaa Peresi na Zera (mama yao alikuwa Tamari), Peresi alimzaa Hesroni, Hesroni alimzaa Rami, Rami alimzaa Aminadabu, Aminadabu alimzaa Nashoni, Nashoni alimzaa Salmoni, Salmoni alimzaa Boazi (mama yake Boazi alikuwa Rahabu) Boazi na Ruthu walikuwa wazazi wa Obedi, Obedi alimzaa Yese, naye Yese alimzaa Mfalme Daudi. Daudi alimzaa Solomoni (mama yake Solomoni alikuwa Bath-Sheba mke wa Uria). Solomoni alimzaa Rehoboamu, Rehoboamu alimzaa Abiya, Abiya alimzaa Asa, Asa alimzaa Yehoshafati, Yehoshafati alimzaa Yoramu, Yoramu alimzaa Uzia, Uzia alimzaa Yothamu, Yothamu alimzaa Ahazi, Ahazi alimzaa Hezekia, Hezekia alimzaa Manase, Manase alimzaa Amoni, Amoni alimzaa Yosia, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake. Huo ulikuwa wakati Wayahudi walipopelekwa uhamishoni Babuloni. Baada ya Wayahudi kupelekwa uhamishoni Babuloni, Yekonia alimzaa Shealtieli, Shealtieli alimzaa Zerubabeli, Zerubabeli alimzaa Abiudi, Abiudi alimzaa Eliakimu, Eliakimu alimzaa Azori, Azori alimzaa Zadoki, Zadoki alimzaa Akimu, Akimu alimzaa Eliudi, Eliudi alimzaa Eleazari, Eleazari alimzaa Mathani, Mathani alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaa Yosefu, mumewe Maria mama yake Yesu aitwaye Kristo. Basi, kulikuwa na vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpaka Wayahudi walipochukuliwa mateka Babuloni, na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwa mateka mpaka wakati wa Kristo.

Shirikisha
Soma Mathayo 1

Mathayo 1:1-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Habari za ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu: Abrahamu akamzaa Isaka, Isaka akamzaa Yakobo, Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake, Yuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari, Peresi akamzaa Esromu, Esromu akamzaa Aramu, Aramu akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nashoni, Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu, Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu, Obedi akamzaa Yese, Yese akamzaa Daudi, aliyekuwa mfalme. Daudi akamzaa Sulemani, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria. Sulemani akamzaa Rehoboamu, Rehoboamu akamzaa Abiya, Abiya akamzaa Asa, Asa akamzaa Yehoshafati, Yehoshafati akamzaa Yoramu, Yoramu akamzaa Uzia, Uzia akamzaa Yothamu, Yothamu akamzaa Ahazi, Ahazi akamzaa Hezekia, Hezekia akamzaa Manase, Manase akamzaa Amoni, Amoni akamzaa Yosia, wakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake. Baada ya uhamisho wa Babeli: Yekonia alimzaa Shealtieli, Shealtieli akamzaa Zerubabeli, Zerubabeli akamzaa Abihudi, Abihudi akamzaa Eliakimu, Eliakimu akamzaa Azori, Azori akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Akimu, Akimu akamzaa Eliudi, Eliudi akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Matani, Matani akamzaa Yakobo, naye Yakobo akamzaa Yusufu, aliyekuwa mumewe Mariamu, mama yake Yesu, aitwaye Kristo. Hivyo, kulikuwa na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu hadi Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho wa Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho wa Babeli hadi Kristo.

Shirikisha
Soma Mathayo 1