Luka 22:67-71
Luka 22:67-71 Biblia Habari Njema (BHN)
Nao wakamwambia, “Tuambie! Je, wewe ndiwe Kristo?” Lakini Yesu akawaambia, “Hata kama nikiwaambieni, hamtasadiki; na hata kama nikiwaulizeni swali, hamtanijibu. Lakini tangu sasa, Mwana wa Mtu atakuwa ameketi upande wa kulia wa Mungu Mwenye Nguvu.” Hapo wote wakasema, “Ndiyo kusema wewe ni Mwana wa Mungu?” Naye akasema, “Nyinyi mnasema kwamba mimi ndiye.” Nao wakasema, “Je, tunahitaji ushahidi mwingine? Sisi wenyewe tumesikia akisema kwa mdomo wake mwenyewe.”
Luka 22:67-71 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie. Akawaambia, Nikiwaambia, hamtasadikia. Tena, nikiwauliza, hamtajibu. Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi. Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye. Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake.
Luka 22:67-71 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie. Akawaambia, Nijapowaambia, hamtasadiki kabisa. Tena, nikiwauliza, hamtajibu. Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi. Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye. Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake.
Luka 22:67-71 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wakamwambia, “Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie.” Yesu akawajibu, “Hata nikiwaambia, hamtaamini. Nami nikiwauliza swali, hamtanijibu. Lakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu ataketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.” Wote wakauliza, “Wewe basi ndiwe Mwana wa Mungu?” Yeye akawajibu, “Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.” Kisha wakasema, “Tuna haja gani tena ya ushahidi zaidi? Tumesikia wenyewe kutoka kinywani mwake.”