Walawi 8:30
Walawi 8:30 Biblia Habari Njema (BHN)
Halafu Mose akachukua mafuta ya kupaka na damu kutoka madhabahu akamnyunyizia Aroni na wanawe hata na pia mavazi yao. Hivyo Mose akamweka wakfu Aroni na wanawe pamoja na mavazi yao.
Walawi 8:30 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha Musa akatwaa baadhi ya mafuta ya kutia, na ya damu iliyokuwa pale juu ya madhabahu, na kumnyunyizia Haruni, katika mavazi yake, na wanawe, katika mavazi yao; akamtakasa Haruni, na mavazi yake, na wanawe, na mavazi ya wanawe waliokuwa pamoja naye.
Walawi 8:30 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha Musa akatwaa baadhi ya mafuta ya kutia, na ya damu iliyokuwa pale juu ya madhabahu, na kumnyunyizia Haruni, katika mavazi yake, na wanawe, katika mavazi yao, pamoja naye; akamtakasa Haruni, na mavazi yake, na wanawe, na mavazi ya wanawe, pamoja naye.
Walawi 8:30 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha Musa akachukua sehemu ya mafuta ya upako, na sehemu ya damu kutoka madhabahu, na kuvinyunyiza juu ya Haruni na mavazi yake, na juu ya wanawe na mavazi yao. Kwa hiyo akamweka Haruni na mavazi yake wakfu, pamoja na wanawe na mavazi yao.