Walawi 7:1-5
Walawi 7:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
“Ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuondoa hatia. Sadaka hiyo ni takatifu kabisa. Mnyama wa sadaka ya kuondoa hatia atachinjiwa mahali wanapochinjiwa wanyama wa sadaka za kuteketezwa, na damu yake itarashiwa madhabahu pande zake zote. Mafuta yake yote: Mafuta ya mkia na yale yanayofunika matumbo yatatolewa na kuteketezwa pamoja na zile figo mbili pamoja na mafuta yake na ile sehemu bora ya ini. Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama sadaka anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Hiyo ni sadaka ya kuondoa hatia.
Walawi 7:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na sheria ya hiyo sadaka ya hatia ni hii; ni takatifu sana. Wataichinja sadaka ya hatia pale pale waichinjapo sadaka ya kuteketezwa; na damu yake atainyunyiza katika madhabahu pande zote. Katika sadaka hiyo atasongeza mafuta yake yote; yaani, mkia wake wenye mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno chake, na kitambi kilicho katika ini, pamoja na figo zake mbili, hayo yote atayaondoa; na kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, kuwa dhabihu kwa BWANA kwa njia ya moto; ni sadaka ya hatia.
Walawi 7:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na sheria ya hiyo sadaka ya hatia ni hii; ni takatifu sana. Wataichinja sadaka ya hatia pale pale waichinjapo sadaka ya kuteketezwa; na damu yake atainyunyiza katika madhabahu pande zote. Katika sadaka hiyo atasongeza mafuta yake yote; yaani, mkia wake wenye mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno chake, na kitambi kilicho katika ini, pamoja na figo zake mbili, hayo yote atayaondoa; na kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, kuwa dhabihu kwa BWANA kwa njia ya moto; ni sadaka ya hatia.
Walawi 7:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“ ‘Haya ndio masharti kwa ajili ya sadaka ya hatia, ambayo ni takatifu sana: Sadaka ya hatia itachinjiwa mahali pale sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa, nayo damu yake itanyunyizwa pande zote za madhabahu. Mafuta yake yote yatatolewa sadaka: mafuta ya mkia, na mafuta yale yanayofunika sehemu za ndani, figo zote mbili pamoja na mafuta yanayozifunika karibu na kiuno, na kipande kirefu cha ini, ambayo yataondolewa pamoja na hizo figo. Kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa BWANA kwa moto. Hii ni sadaka ya hatia.