Walawi 4:1-12
Walawi 4:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Waambie watu wa Israeli hivi: Kama mtu ametenda dhambi bila kukusudia, akafanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu, atafanya kama ifuatavyo: Ikiwa kuhani ambaye amepakwa mafuta ndiye aliyetenda dhambi hata akawatia watu hatiani, basi huyo atamtolea Mwenyezi-Mungu fahali mchanga asiye na dosari awe sadaka ya kuondoa dhambi. Atamleta huyo fahali mchanga kwenye mlango wa hema la mkutano, mbele ya Mwenyezi-Mungu; naye ataweka mkono wake juu ya kichwa cha fahali huyo na kumchinja mbele ya Mwenyezi-Mungu. Huyo kuhani, aliyepakwa mafuta atachukua kiasi cha damu na kuingia nayo ndani ya hema la mkutano. Atachovya kidole chake katika damu hiyo na kuirashia mara saba mbele ya Mwenyezi-Mungu upande wa mbele wa pazia la mahali patakatifu. Kuhani atachukua sehemu ya damu na kuzipaka pembe za madhabahu ya kufukizia ubani wa harufu nzuri, mbele ya Mwenyezi-Mungu katika hema la mkutano. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka iliyoko karibu na mlango wa hema la mkutano. Kisha atayaondoa mafuta yote ya ng'ombe huyo: Mafuta yanayofunika matumbo, figo mbili na mafuta yaliyo juu yake na yale yaliyo kiunoni, na yale yaliyoshikamana na figo na ini; hizi ni sehemu zilezile zinazoondolewa kwa mnyama wa sadaka ya amani. Kuhani atazichukua na kuziteketeza juu ya madhabahu ya kuteketezea sadaka. Lakini ngozi ya huyo ng'ombe, nyama, kichwa, miguu, matumbo na mavi yake, yaani ng'ombe mzima aliyesalia atampeleka na kumteketeza nje ya kambi mahali safi ambapo majivu hutupwa, naye atamchoma kwa moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo mahali pa kumwagia majivu.
Walawi 4:1-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu yeyote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lolote ambalo BWANA amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lolote la maneno hayo; kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng'ombe dume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi. Naye atamleta huyo ng'ombe na kumweka mlangoni pa hiyo hema ya kukutania, mbele za BWANA; naye ataweka mkono wake kichwani mwake ng'ombe, na kumchinja huyo ng'ombe mbele za BWANA. Kisha huyo kuhani aliyetiwa mafuta atatwaa baadhi ya damu ya huyo ng'ombe, na kuileta ndani ya hiyo hema ya kukutania; kisha kuhani atatia kidole chake katika hiyo damu na kuinyunyiza damu mbele ya BWANA mara saba, mbele ya pazia la mahali patakatifu. Kisha kuhani atatia baadhi ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba mzuri mbele ya BWANA iliyo ndani ya hema ya kukutania; kisha damu yote ya huyo ng'ombe ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyoko mlangoni pa hema ya kukutania. Kisha mafuta yote ya huyo ng'ombe wa sadaka ya dhambi atayaondoa; mafuta yote yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo, na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno chake, na kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo, hayo yote atayaondoa, vile vile kama yanavyoondolewa katika ng'ombe wa kuchinjwa kwa sadaka za amani; kisha huyo kuhani atayateketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Kisha ngozi yake ng'ombe, na nyama yake yote, pamoja na kichwa chake, na pamoja na miguu yake, na matumbo yake, na mavi yake, maana, huyo ng'ombe mzima atamchukua nje ya kambi hata mahali safi, hapo wamwagapo majivu, naye atamchoma moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo majivu yamwagwapo.
Walawi 4:1-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu ye yote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lo lote ambalo BWANA amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lo lote la maneno hayo; kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng’ombe mume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi. Naye atamleta huyo ng’ombe na kumweka mlangoni pa hiyo hema ya kukutania, mbele za BWANA; naye ataweka mkono wake kichwani mwake ng’ombe, na kumchinja huyo ng’ombe mbele za BWANA. Kisha huyo kuhani aliyetiwa mafuta atatwaa baadhi ya damu ya huyo ng’ombe, na kuileta ndani ya hiyo hema ya kukutania; kisha kuhani atatia kidole chake katika hiyo damu na kuinyunyiza damu mbele ya BWANA mara saba, mbele ya pazia la mahali patakatifu. Kisha kuhani atatia baadhi ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba mzuri mbele ya BWANA iliyo ndani ya hema ya kukutania; kisha damu yote ya huyo ng’ombe ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyoko mlangoni pa hema ya kukutania. Kisha mafuta yote ya huyo ng’ombe wa sadaka ya dhambi atayaondoa; mafuta yote yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo, na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno chake, na kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo, hayo yote atayaondoa, vile vile kama yanavyoondolewa katika ng’ombe wa kuchinjwa kwa sadaka za amani; kisha huyo kuhani atayateketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Kisha ngozi yake ng’ombe, na nyama yake yote, pamoja na kichwa chake, na pamoja na miguu yake, na matumbo yake, na mavi yake, maana, huyo ng’ombe mzima atamchukua nje ya marago hata mahali safi, hapo wamwagapo majivu, naye atamchoma moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo majivu yamwagwapo.
Walawi 4:1-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA akamwambia Musa, “Waambie Waisraeli: ‘Mtu yeyote afanyapo dhambi bila kukusudia na akatenda lile lililokatazwa katika amri yoyote ya BWANA: “ ‘Ikiwa kuhani aliyepakwa mafuta amefanya dhambi na kuwaletea watu hatia, lazima alete kwa BWANA fahali mchanga asiye na dosari, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya dhambi aliyotenda. Atamkabidhi huyo fahali kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za BWANA. Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha huyo fahali na kumchinja mbele za BWANA. Kisha kuhani huyo aliyepakwa mafuta atachukua sehemu ya damu ya huyo fahali na kuileta katika Hema la Kukutania. Atachovya kidole chake katika hiyo damu, na kuinyunyiza sehemu yake mara saba mbele za BWANA, mbele ya pazia la mahali patakatifu. Kisha kuhani atatia sehemu ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba wenye harufu nzuri iliyo mbele za BWANA katika Hema la Kukutania. Damu iliyobaki ya huyo fahali ataimwaga chini ya hayo madhabahu ya kuteketezea sadaka kwenye ingilio la Hema la Kukutania. Atayaondoa mafuta yote ya fahali huyo wa sadaka ya dhambi: mafuta yale yanayofunika sehemu za ndani au zile zinazounganika nazo, figo zote mbili na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno, na kipande kirefu cha ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo zote, kama vile mafuta yanavyoondolewa kutoka kwa ngʼombe aliyetolewa sadaka ya amani. Kisha kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Lakini ngozi ya huyo fahali na nyama zake zote, pamoja na kichwa na miguu yake, sehemu za ndani na matumbo, yaani sehemu nyingine zote zilizobaki za huyo fahali, lazima azitoe nje ya kambi hadi mahali palipo safi, ambapo majivu hutupwa; naye atamchoma kwa moto wa kuni juu ya lundo la majivu.