Walawi 20:6-8
Walawi 20:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
“Kama mtu yeyote anawaendea waaguzi wa mizimu na wachawi na hivyo kukosa uaminifu kwangu, nitamkabili mtu huyo na kumtenga na watu wake. Kwa hiyo, jiwekeni wakfu muwe watakatifu; kwani mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Shikeni masharti yangu na kuyatekeleza. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu ninayewatakasa.
Walawi 20:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake. Jitakaseni basi, kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Nanyi zishikeni sheria zangu, na kuzitenda; Mimi ndimi BWANA niwatakasaye.
Walawi 20:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake. Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Nanyi zishikeni sheria zangu, na kuzitenda; Mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi.
Walawi 20:6-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“ ‘Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu anayeenda kwa waaguzi na wenye pepo, na hivyo kujifanyia ukahaba kwa kuwafuata, nami nitamkatilia mbali na watu wake. “ ‘Jitakaseni basi, nanyi kuweni watakatifu, kwa sababu mimi ndimi BWANA Mungu wenu. Shikeni amri zangu na kuzifuata. Mimi ndimi BWANA, niwafanyaye ninyi watakatifu.