Walawi 19:26-28
Walawi 19:26-28 Biblia Habari Njema (BHN)
“Msile nyama yoyote yenye damu. Msipige bao wala kufanya uchawi. Nywele zenu msizikate pembeni wala kunyoa ndevu zenu. Msijitie alama zozote mwilini mwenu kwa ajili ya kuomboleza au kujikatakata mwilini au kujichanja chale. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Walawi 19:26-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Msile kitu chochote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi. Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu. Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA.
Walawi 19:26-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi. Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu. Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA.
Walawi 19:26-28 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“ ‘Msile nyama yoyote yenye damu ndani yake. “ ‘Msifanye uaguzi wala uchawi. “ ‘Msikate nywele za kichwa denge, wala kunyoa pembe za ndevu zenu. “ ‘Msichanje chale miili yenu kwa ajili ya mfu, wala msijichore alama juu ya miili yenu. Mimi ndimi BWANA.