Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Walawi 19:23-24 - Compare All Versions

Walawi 19:23-24 BHN (Biblia Habari Njema)

“Mtakapofika katika nchi ya Kanaani na kupanda aina zote za miti ya matunda, matunda hayo hamtayala; hamtaruhusiwa kuyala kwa muda wa miaka mitatu. Mnamo mwaka wa nne matunda yake yote yatakuwa matakatifu, yatatolewa kuwa sadaka ya sifa, kwa Mwenyezi-Mungu.

Shirikisha
Walawi 19 BHN

Walawi 19:23-24 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Nanyi mtakapoingia katika nchi ile, na kupanda miti ya namna zote kwa ajili ya chakula, ndipo mtayahesabu matunda yake kama yaliyotakazwa; kwa muda wa miaka mitatu miti hiyo itakuwa kwenu kama katazo; matunda yake hayataliwa. Lakini mwaka wa nne matunda yake yote yatakuwa ni matakatifu, kwa ajili ya kumpa BWANA shukrani.

Shirikisha
Walawi 19 SRUV

Walawi 19:23-24 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Nanyi hapo mtakapoingia nchi ile, mkiwa mmepanda miti ya namna zote kwa ajili ya chakula, ndipo mtayahesabu matunda yake kama ni kutotahiriwa; muda wa miaka mitatu miti hiyo itakuwa kwenu kama kutotahiriwa; matunda yake hayataliwa. Lakini mwaka wa nne matunda yake yote yatakuwa ni matakatifu, kwa ajili ya kumpa BWANA shukrani.

Shirikisha
Walawi 19 SUV

Walawi 19:23-24 NEN (Neno)

“ ‘Mtakapoingia katika hiyo nchi na kupanda aina yoyote ya mti wa matunda, hesabuni matunda yake kama yaliyokatazwa. Kwa miaka mitatu mtayahesabu kwamba yamekatazwa; hayaruhusiwi kuliwa. Katika mwaka wa nne matunda yote ya mti huo yatakuwa matakatifu, sadaka ya sifa kwa BWANA.

Shirikisha
Walawi 19 NEN