Walawi 19:13-14
Walawi 19:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
“Usimdhulumu jirani yako wala kumwibia. Mshahara wa mtu aliyeajiriwa usikae kwako usiku kucha hadi asubuhi. Usimlaani kiziwi wala kuweka kizuizi mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Walawi 19:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usimdhulumu jirani yako, wala kumnyang'anya mali yake; ujira wake aliyeajiriwa usikae kwako usiku kucha hadi asubuhi. Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi BWANA.
Walawi 19:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usimdhulumu jirani yako, wala kumnyang’anya mali yake; ijara yake aliyeajiriwa isikae kwako usiku kucha hata asubuhi. Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi BWANA.