Walawi 12:2-5
Walawi 12:2-5 Biblia Habari Njema (BHN)
“Waambie watu wa Israeli hivi: Mwanamke akipata mimba, akajifungua mtoto wa kiume, atakuwa najisi kwa muda wa siku saba kulingana na siku zake zihusikanazo na hali ya wanawake. Mtoto huyo atatahiriwa katika siku yake ya nane. Kisha mama mtoto ataendelea kuwa najisi kwa muda wa siku thelathini na tatu. Wakati huo, kamwe asiguse chochote kilichowekwa wakfu wala kuingia mahali patakatifu mpaka siku za kutakasika kwake zitakapotimia. Lakini, kama amejifungua mtoto wa kike, basi, atakuwa najisi kwa muda wa majuma mawili kama ilivyo anapokuwa katika siku zake. Ataendelea katika kutakasika kwake kwa muda wa siku sitini na sita.
Walawi 12:2-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto wa kiume, ndipo atakuwa najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi ndivyo atakavyokuwa najisi. Siku ya nane mtoto atatahiriwa govi ya zunga lake. Na huyo mwanamke atakaa muda wa siku thelathini na tatu ili kutakata damu yake. Lakini kama amezaa mtoto wa kike naye atakaa muda wa siku sitini na sita ili kutakata damu yake.
Walawi 12:2-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto mume, ndipo atakuwa yu najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi, ndivyo atakavyokuwa najisi. Siku nane mtoto atatahiriwa govi ya zunga lake. Na huyo mwanamke atakaa katika damu ya kutakata kwake siku thelathini na tatu; asiguse kitu kilicho kitakatifu, wala asiingie mahali patakatifu, hata siku hizo za kutakata kwake zitakapotimia. Lakini kwamba amezaa mtoto mke ndipo atakuwa najisi juma mbili, kama katika kutengwa kwake; naye atakaa katika damu ya kutakata kwake muda wa siku sitini na sita.
Walawi 12:2-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Waambie Waisraeli: ‘Mwanamke ambaye atapata mimba na kuzaa mtoto wa kiume atakuwa najisi kwa siku saba, kama anavyokuwa najisi wakati wa siku zake za hedhi. Naye huyo mtoto atatahiriwa siku ya nane. Kisha ni lazima huyo mwanamke asubiri kwa siku thelathini na tatu, ndipo atakaswe kutoka damu kwake. Hataruhusiwa kugusa kitu chochote kilicho kitakatifu au kuingia mahali patakatifu, hadi siku za kutakaswa kwake zimetimia. Kama alimzaa mtoto wa kike, mwanamke huyo atakuwa najisi kwa majuma mawili, kama wakati wake wa hedhi. Kisha atasubiri kwa siku sitini na sita, ndipo atatakaswa kutoka damu kwake.