Walawi 1:1-4
Walawi 1:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu alimwita Mose na kuongea naye katika hema la mkutano, akamwambia, “Waambie Waisraeli kwamba kama mtu anapenda kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya mnyama, mnyama huyo atamchagua kutoka kundi lake la ng'ombe, kondoo au mbuzi. “Kama sadaka anayotoa mtu ni ya kuteketezwa, atamchagua mnyama dume asiye na dosari kutoka kundi lake, atamtolea mbele ya mlango wa hema la mkutano ili apate fadhili ya Mwenyezi-Mungu; ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka ya kuteketezwa, ambayo itakubaliwa kwa ajili ya kumfanyia huyo mtu upatanisho.
Walawi 1:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea BWANA matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa kufugwa, katika ng'ombe, kondoo na mbuzi. Ikawa matoleo yake ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe dume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA. Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.
Walawi 1:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea BWANA matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng’ombe na katika kondoo. Matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng’ombe, atatoa ng’ombe mume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA. Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.
Walawi 1:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA akamwita Musa na kusema naye kutoka Hema la Kukutania, akamwambia, “Sema na Waisraeli, uwaambie, ‘Yeyote miongoni mwenu anayeleta sadaka kwa BWANA, alete mnyama kama sadaka yake kutoka kundi lake la ngʼombe, au la kondoo na mbuzi. “ ‘Ikiwa sadaka hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kutoka kundi la ngʼombe, atamtoa ngʼombe dume asiye na dosari. Ni lazima amlete kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili aweze kukubalika kwa BWANA. Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa niaba yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.