Walawi 1:1-2
Walawi 1:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu alimwita Mose na kuongea naye katika hema la mkutano, akamwambia, “Waambie Waisraeli kwamba kama mtu anapenda kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya mnyama, mnyama huyo atamchagua kutoka kundi lake la ng'ombe, kondoo au mbuzi.
Walawi 1:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea BWANA matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa kufugwa, katika ng'ombe, kondoo na mbuzi.
Walawi 1:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea BWANA matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng’ombe na katika kondoo.
Walawi 1:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA akamwita Musa na kusema naye kutoka Hema la Kukutania, akamwambia, “Sema na Waisraeli, uwaambie, ‘Yeyote miongoni mwenu anayeleta sadaka kwa BWANA, alete mnyama kama sadaka yake kutoka kundi lake la ngʼombe, au la kondoo na mbuzi.