Maombolezo 4:1-22
Maombolezo 4:1-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Jinsi gani dhahabu yetu ilivyochujuka, dhahabu safi kabisa ilivyobadilika! Mawe ya thamani yametawanywa yamesambaa barabarani kote. Watoto wa Siyoni waliosifika sana, waliothaminiwa kama dhahabu safi, jinsi gani sasa wamekuwa kama vyombo vya udongo, kazi ya mikono ya mfinyanzi! Hata mbwamwitu huwa na hisia za mama na kuwanyonyesha watoto wao; lakini watu wangu wamekuwa wakatili, hufanya kama mbuni nyikani. Midomo ya watoto wachanga imekauka kwa kiu, watoto wanaomba chakula lakini hakuna anayewapa. Watu waliojilisha vyakula vinono sasa wanakufa njaa barabarani. Waliolelewa na kuvikwa kifalme sasa wanafukua kwa mikono kwenye majaa. Watu wangu wamepata adhabu kubwa kuliko watu wa mji wa Sodoma mji ambao uliteketezwa ghafla bila kuwa na muda wa kunyosha mkono. Vijana wa Siyoni walikuwa safi kuliko theluji, walikuwa weupe kuliko maziwa. Miili yao ilikuwa myekundu kama matumbawe, uzuri wa viwiliwili vyao kama johari ya rangi ya samawati. Sasa sura zao ni nyeusi kuliko makaa, wanapita barabarani bila kujulikana; ngozi yao imegandamana na mifupa yao imekauka, imekuwa kama kuni. Afadhali waliouawa kwa upanga kuliko waliokufa kwa njaa, ambao walikufa polepole kwa kukosa chakula. Kina mama ambao huwa na huruma kuu waliwapika watoto wao wenyewe, wakawafanya kuwa chakula chao wakati watu wangu walipoangamizwa. Mwenyezi-Mungu alionesha uzito wa ghadhabu yake, aliimimina hasira yake kali; aliwasha moto huko mjini Siyoni ambao uliteketeza misingi yake. Wafalme duniani hawakuamini wala wakazi wowote wa ulimwenguni, kwamba mvamizi au adui angeweza kuingia malango ya Yerusalemu. Hayo yalisababishwa na dhambi za manabii wake, yalitukia kwa sababu ya uovu wa makuhani wake ambao walimwaga damu ya waadilifu mjini kwake. Walitangatanga barabarani kama vipofu, walikuwa wamekuwa najisi kwa damu, hata asiwepo mtu yeyote wa kuwagusa. Watu waliwapigia kelele wakisema: “Tokeni, nendeni zenu enyi mlio najisi! Tokeni, tokeni, msiguse chochote.” Hivyo wakawa wakimbizi na kutangatanga; watu wa mataifa walitamka: “Hawa hawatakaribishwa kukaa kwetu!” Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwatawanya, wala hatawajali tena. Makuhani hawatapata tena heshima, wazee hawatapendelewa tena. Tulichoka kukaa macho kungojea msaada; tulikesha na kungojea kwa hamu taifa ambalo halikuweza kutuokoa. Watu walifuatilia hatua zetu, tukashindwa kupita katika barabara zetu. Siku zetu zikawa zimetimia; mwisho wetu ukawa umefika. Waliotufuatia walikuwa wepesi kuliko tai, walitukimbiza milimani, walituvizia huko nyikani. Walimnasa yule ambaye maisha yetu yalimtegemea, yule mfalme aliyewekwa wakfu wa Mwenyezi-Mungu, yule ambaye tulisema: “Chini ya ulinzi wake tutaishi miongoni mwa mataifa.” Wakazi wa Edomu, mwaweza kushangilia kwa sasa, mwaweza kwa sasa kufurahi enyi wakazi wa Uzi; lakini kikombe hiki cha adhabu kitawajia pia, nanyi pia mtakinywa na kulewa, hata mtayavua mavazi yenu! Adhabu ya uovu wako ewe Siyoni imekamilika; Mwenyezi-Mungu hatawaacha zaidi uhamishoni. Lakini nyinyi Waedomu atawaadhibu kwa uovu wenu, atazifichua dhambi zenu.
Maombolezo 4:1-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Jinsi dhahabu ilivyoacha kung'aa, Na dhahabu iliyo safi ilivyobadilika! Mawe ya patakatifu yametupwa Mwanzo wa kila njia. Wana wa Sayuni wenye thamani, Walinganao na dhahabu safi, Jinsi wanavyodhaniwa kuwa vyombo vya udongo, Kazi ya mikono ya mfinyanzi! Hata mbwamwitu hutoa matiti, Huwanyonyesha watoto wao; Binti ya watu wangu amekuwa mkali, Mfano wa mbuni jangwani. Ulimi wa mtoto anyonyaye Wagandamana na kinywa chake kwa kiu; Watoto wachanga waomba chakula, Wala hakuna hata mmoja awamegeaye. Wale waliokula vitu vya anasa Wameachwa peke yao njiani; Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekundu Wakumbatia jaa. Maana uovu wa binti ya watu wangu ni mkubwa Kuliko dhambi ya Sodoma, Uliopinduliwa kama katika dakika moja, Wala mikono haikuwekwa juu yake. Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji, Walikuwa weupe kuliko maziwa; Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani, Na umbo lao kama yakuti samawi. Nyuso zao ni nyeusi kuliko makaa; Hawajulikani katika njia kuu; Ngozi yao yagandamana na mifupa yao Imekauka, imekuwa kama mti. Heri wale waliouawa kwa upanga Kuliko wao waliouawa kwa njaa; Maana hao husinyaa, wakichomwa Kwa kukosa matunda ya mashamba. Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu. BWANA ameitimiza ghadhabu yake, Ameimimina hasira yake kali; Naye amewasha moto katika Sayuni Ulioiteketeza misingi yake. Wafalme wa dunia hawakusadiki, Wala wote wakaao duniani, Ya kwamba mtesi na adui wangeingia Katika malango ya Yerusalemu. Ni kwa sababu ya dhambi za manabii wake Na maovu ya makuhani wake, Walioimwaga damu ya wenye haki Katikati yake. Hutangatanga njiani kama vipofu, Wametiwa unajisi kwa damu; Hata ikawa hakuna aliyeweza Kuyagusa mavazi yao. Watu waliwapigia kelele, Ondokeni, Uchafu, Ondokeni, ondokeni, msiguse; Walipokimbia na kutangatanga, watu walisema kati ya mataifa, Hawatakaa hapa tena. Hasira ya BWANA imewatenga, Yeye hatawaangalia tena; Hawakujali nafsi za wale makuhani, Hawakuwaheshimu wazee wao. Macho yetu yamechoka Kwa kuutazamia bure msaada wetu; Katika kungoja kwetu tumengojea taifa Lisiloweza kutuokoa. Wanatuvizia hatua zetu, Hata hatuwezi kwenda katika njia zetu; Mwisho wetu umekaribia, siku zetu zimetimia; Maana mwisho wetu umefika. Waliotufuatia ni wepesi Kuliko tai za mbinguni; Hao walitufuatia milimani, Nao walituotea jangwani. Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao; Ambaye kwa habari zake tulisema, Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa. Furahi, ushangilie, Ee binti Edomu, Ukaaye katika nchi ya Usi; Hata kwako kikombe kitapita, Utalewa, na kujifanya uchi. Adhabu ya uovu wako imetimia, Ee binti Sayuni; Hatakuhamisha tena; Atapatiliza uovu wako, Ee binti Edomu; Atazivumbua dhambi zako.
Maombolezo 4:1-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jinsi dhahabu ilivyoacha kung’aa, Na dhahabu iliyo safi ilivyobadilika! Mawe ya patakatifu yametupwa Mwanzo wa kila njia. Wana wa Sayuni wenye thamani, Walinganao na dhahabu safi, Jinsi wanavyodhaniwa kuwa vyombo vya udongo, Kazi ya mikono ya mfinyanzi! Hata mbwa-mwitu hutoa matiti, Huwanyonyesha watoto wao; Binti ya watu wangu amekuwa mkali, Mfano wa mbuni jangwani. Ulimi wa mtoto anyonyaye Wagandamana na kaakaa lake kwa kiu; Watoto wachanga waomba chakula, Wala hakuna hata mmoja awamegeaye. Wale waliokula vitu vya anasa Wameachwa peke yao njiani; Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekundu Wakumbatia jaa. Maana uovu wa binti ya watu wangu ni mkubwa Kuliko dhambi ya Sodoma, Uliopinduliwa kama katika dakika moja, Wala mikono haikuwekwa juu yake. Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji, Walikuwa weupe kuliko maziwa; Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani, Na umbo lao kama yakuti samawi. Nyuso zao ni nyeusi kuliko makaa; Hawajulikani katika njia kuu; Ngozi yao yagandamana na mifupa yao Imekauka, imekuwa kama mti. Heri wale waliouawa kwa upanga Kuliko wao waliouawa kwa njaa; Maana hao husinyaa, wakichomwa Kwa kukosa matunda ya mashamba. Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu. BWANA ameitimiza kani yake, Ameimimina hasira yake kali; Naye amewasha moto katika Sayuni Ulioiteketeza misingi yake. Wafalme wa dunia hawakusadiki, Wala wote wakaao duniani, Ya kwamba mtesi na adui wangeingia Katika malango ya Yerusalemu. Ni kwa sababu ya dhambi za manabii wake Na maovu ya makuhani wake, Walioimwaga damu ya wenye haki Katikati yake. Hutanga-tanga njiani kama vipofu, Wametiwa unajisi kwa damu; Hata ikawa watu wasiweze Kuyagusa mavazi yao. Watu waliwapigia kelele, Ondokeni, Uchafu, Ondokeni, ondokeni, msiguse; Walipokimbia na kutanga-tanga, watu walisema kati ya mataifa, Hawatakaa hapa tena. Hasira ya BWANA imewatenga, Yeye hatawaangalia tena; Hawakujali nafsi za wale makuhani, Hawakuwaheshimu wazee wao. Macho yetu yamechoka Kwa kuutazamia bure msaada wetu; Katika kungoja kwetu tumengojea taifa Lisiloweza kutuokoa. Wanatuvizia hatua zetu, Hata hatuwezi kwenda katika njia zetu; Mwisho wetu umekaribia, siku zetu zimetimia; Maana mwisho wetu umefika. Waliotufuatia ni wepesi Kuliko tai za mbinguni; Hao walitufuatia milimani, Nao walituotea jangwani. Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao; Ambaye kwa habari zake tulisema, Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa. Furahi, ushangilie, Ee binti Edomu, Ukaaye katika nchi ya Usi; Hata kwako kikombe kitapita, Utalewa, na kujifanya uchi. Uovu wako umetimia, Ee binti Sayuni; Hatakuhamisha tena; Atapatiliza uovu wako, Ee binti Edomu; Atazivumbua dhambi zako.
Maombolezo 4:1-22 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Jinsi dhahabu ilivyopoteza mngʼao wake, dhahabu iliyo safi haingʼai! Vito vya thamani vimetawanywa kwenye mwanzo wa kila barabara. Wana wa Sayuni wenye thamani, ambao mwanzo uzito wa thamani yao ulikuwa wa dhahabu, sasa wanaangaliwa kama vyungu vya udongo, kazi ya mikono ya mfinyanzi! Hata mbweha hutoa matiti yao kunyonyesha watoto wao, lakini watu wangu wamekuwa wasio na huruma kama mbuni jangwani. Kwa sababu ya kiu ulimi wa mtoto mchanga umegandamana na kaakaa la kinywa chake, watoto huomba mkate, lakini hakuna yeyote awapaye. Wale waliokula vyakula vya kifahari ni maskini barabarani. Wale waliokuzwa wakivaa nguo za zambarau sasa wanalalia majivu. Adhabu ya watu wangu ni kubwa kuliko ile ya Sodoma, ambayo ilipinduliwa ghafula wala hapakuwa na mkono wa msaada. Wakuu wao walikuwa wamengʼaa kuliko theluji na weupe kuliko maziwa, miili yao ilikuwa myekundu kuliko marijani, kuonekana kwao kama yakuti samawi. Lakini sasa ni weusi kuliko masizi; hawatambulikani barabarani. Ngozi yao imeshikamana juu ya mifupa yao, imekuwa mikavu kama fimbo. Wale waliouawa kwa upanga ni bora kuliko wale wanaokufa njaa; wanateseka kwa njaa, wanatokomea kwa kukosa chakula kutoka shambani. Kwa mikono yao wenyewe wanawake wenye huruma wanapika watoto wao wenyewe, waliokuwa chakula chao watu wangu walipoangamizwa. BWANA ametoa nafasi kamilifu ya ghadhabu yake; ameimwaga hasira yake kali. Amewasha moto katika Sayuni ambao umeteketeza misingi yake. Wafalme wa dunia hawakuamini, wala mtu yeyote wa duniani, kwamba adui na watesi wangeweza kuingia kwenye malango ya Yerusalemu. Lakini hili lilitokea kwa sababu ya dhambi za manabii wake, na maovu ya makuhani wake, waliomwaga ndani yake damu ya wenye haki. Sasa wanapapasa papasa barabarani kama watu ambao ni vipofu. Wamenajisiwa kabisa kwa damu, hata hakuna anayethubutu kugusa mavazi yao. Watu wanawapigia kelele, “Ondokeni! Ninyi ni najisi! Ondokeni! Ondokeni! Msituguse!” Wanapokimbia na kutangatanga, watu miongoni mwa mataifa wanasema, “Hawawezi kukaa hapa zaidi.” BWANA mwenyewe amewatawanya; hawaangalii tena. Makuhani hawaoneshwi heshima, wazee hawakubaliki. Zaidi ya hayo, macho yetu yalichoka, kwa kutazamia bure msaada; tuliangalia kutoka minara yetu kwa taifa lisiloweza kutuokoa. Watu walituvizia katika kila hatua hata hatukuweza kutembea katika barabara zetu. Mwisho wetu ulikuwa karibu, siku zetu zilikuwa zimetimia, kwa maana mwisho wetu ulikuwa umefika. Waliotufuatia walikuwa wepesi kuliko tai angani; walitusaka juu milimani na kutuvizia jangwani. Mpakwa mafuta wa BWANA, pumzi ya uhai wetu hasa, alinaswa katika mitego yao. Tulifikiri kwamba chini ya kivuli chake tungeishi miongoni mwa mataifa. Shangilia na ufurahi, ee Binti Edomu, wewe unayeishi nchi ya Usi. Lakini kwako pia kikombe kitapitishwa, Utalewa na kuvuliwa nguo ubaki uchi. Ee Binti Sayuni, adhabu yako itaisha, hatarefusha muda wako wa kukaa uhamishoni. Lakini, ee Binti Edomu, ataadhibu dhambi yako, na atafunua uovu wako.