Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombolezo 3:4-6 - Compare All Versions

Maombolezo 3:4-6 BHN (Biblia Habari Njema)

Amenichakaza ngozi na nyama, mifupa yangu ameivunja. Amenizingira na kunizungushia uchungu na mateso. Amenikalisha gizani kama watu waliokufa zamani.

Maombolezo 3:4-6 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Amechakaza nyama yangu na ngozi yangu; Ameivunja mifupa yangu. Amejenga boma juu yangu, Na kunizungusha uchungu na uchovu. Amenikalisha penye giza, Kama watu waliokufa zamani.

Maombolezo 3:4-6 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Amechakaza ngozi yangu na nyama yangu; Ameivunja mifupa yangu. Amejenga boma juu yangu, Na kunizungusha uchungu na uchovu. Amenikalisha penye giza, Kama watu waliokufa zamani.

Maombolezo 3:4-6 NEN (Neno)

Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa na ameivunja mifupa yangu. Amenizingira na kunizunguka kwa uchungu na taabu. Amenifanya niishi gizani kama wale waliokufa.