Maombolezo 3:34-44
Maombolezo 3:34-44 Biblia Habari Njema (BHN)
Wafungwa wote nchini wanapodhulumiwa na kupondwa; haki za binadamu zinapopotoshwa mbele yake Mungu Mkuu, kesi ya mtu inapopotoshwa mahakamani, je, Mwenyezi-Mungu haoni hayo? Nani awezaye kuamuru kitu kifanyike Mwenyezi-Mungu asipopanga iwe hivyo? Maafa na mema hutokea tu kwa amri yake Mungu Mkuu. Kwa nini mtu anung'unike, ikiwa ameadhibiwa kwa dhambi zake? Na tupime na kuchunguza mwenendo wetu, tupate kumrudia Mwenyezi-Mungu. Tumfungulie Mungu huko mbinguni mioyo yetu na kumwomba: “Sisi tulikukosea na kukuasi nawe bado hujatusamehe. “Umejizungushia hasira yako ukatufuatia, ukatuua bila huruma. Umejizungushia wingu zito, sala yeyote isiweze kupenya humo.
Maombolezo 3:34-44 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wafungwa wote wa duniani Kupondwa chini kwa miguu, Kuipotosha hukumu ya mtu Mbele zake Aliye Juu, Na kumnyima mtu haki yake, Hayo Bwana hayaridhii kabisa. Ni nani asemaye neno nalo likafanyika, Ikiwa Bwana hakuliagiza? Je! Katika kinywa chake Aliye Juu Hayatoki maovu na mema? Mbona anung'unika mwanadamu aliye hai Mtu akiadhibiwa kwa dhambi zake? Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu, Na kumrudia BWANA tena. Na tumwinulie Mungu aliye mbinguni Mioyo yetu na mikono. Sisi tumekosa na kuasi; Wewe hukusamehe. Umetufunika kwa hasira na kutufuatia; Umeua, wala hukuona huruma. Umejifunika nafsi yako kwa wingu, Maombi yetu yasipite.
Maombolezo 3:34-44 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kuwaseta chini kwa miguu Wafungwa wote wa duniani, Kuipotosha hukumu ya mtu Mbele zake Aliye juu, Na kumnyima mtu haki yake, Hayo Bwana hayaridhii kabisa. Ni nani asemaye neno nalo likafanyika, Ikiwa Bwana hakuliagiza? Je! Katika kinywa chake Aliye juu Hayatoki maovu na mema? Mbona anung’unika mwanadamu aliye hai Mtu akiadhibiwa kwa dhambi zake? Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu, Na kumrudia BWANA tena. Na tumwinulie Mungu aliye mbinguni Mioyo yetu na mikono. Sisi tumekosa na kuasi; Wewe hukusamehe. Umetufunika kwa hasira na kutufuatia; Umeua, wala hukuona huruma. Umejifunika nafsi yako kwa wingu, Maombi yetu yasipite.
Maombolezo 3:34-44 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kuwaponda chini ya nyayo wafungwa wote katika nchi, Kumnyima mtu haki zake mbele za Aliye Juu Sana, kumnyima mtu haki: Je, Bwana asione mambo kama haya? Nani awezaye kusema nalo likatendeka kama Bwana hajaamuru? Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sana ndiko yatokako maafa na mambo mema? Je, mwanadamu yeyote aliye hai aweza kulalamika wakati anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake? Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie BWANA Mungu. Tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetu kwa Mungu mbinguni, na tuseme: “Tumetenda dhambi na kuasi nawe hujasamehe. “Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia; umetuchinja bila huruma. Unajifunika mwenyewe kwa wingu, ili pasiwe na ombi litakaloweza kupenya.