Maombolezo 3:3-6
Maombolezo 3:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Amenyosha mkono wake dhidi yangu mimi tu, akanichapa tena na tena mchana kutwa. Amenichakaza ngozi na nyama, mifupa yangu ameivunja. Amenizingira na kunizungushia uchungu na mateso. Amenikalisha gizani kama watu waliokufa zamani.
Maombolezo 3:3-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hakika juu yangu augeuza mkono wake Mara kwa mara mchana wote. Amechakaza ngozi yangu na nyama yangu; Ameivunja mifupa yangu. Amejenga boma juu yangu, Na kunizungusha uchungu na uchovu. Amenikalisha penye giza, Kama watu waliokufa zamani.
Maombolezo 3:3-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hakika juu yangu augeuza mkono wake Mara kwa mara mchana wote. Amechakaza nyama yangu na ngozi yangu; Ameivunja mifupa yangu. Amejenga boma juu yangu, Na kunizungusha uchungu na uchovu. Amenikalisha penye giza, Kama watu waliokufa zamani.
Maombolezo 3:3-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu tena na tena, mchana kutwa. Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa na ameivunja mifupa yangu. Amenizingira na kunizunguka kwa uchungu na taabu. Amenifanya niishi gizani kama wale waliokufa.