Maombolezo 3:19-25
Maombolezo 3:19-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Kukumbuka taabu na kutangatanga kwangu kwanipa uchungu kama wa nyongo. Nayafikiria hayo daima, nayo roho yangu imejaa majonzi. Lakini nakumbuka jambo hili moja, nami ninalo tumaini: Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi, huruma zake hazina mwisho. Kila kunapokucha ni mpya kabisa, uaminifu wake ni mkuu mno. Mwenyezi-Mungu ndiye hazina yangu hivyo nitamwekea tumaini langu. Mwenyezi-Mungu ni mwema kwa wanaomtegemea, ni mwema kwa wote wanaomtafuta.
Maombolezo 3:19-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu, Pakanga na nyongo. Nafsi yangu ingali ikiyakumbuka hayo, Nayo imeinama ndani yangu. Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini. Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye. BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
Maombolezo 3:19-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu, Pakanga na nyongo. Nafsi yangu ikali ikiyakumbuka hayo, Nayo imeinama ndani yangu. Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini. Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye. BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
Maombolezo 3:19-25 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu, uchungu na nyongo. Ninayakumbuka vyema, nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu. Hata hivyo najikumbusha neno hili na kwa hiyo ninalo tumaini. Kwa sababu ya upendo mkuu wa BWANA, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu. Nimeiambia nafsi yangu, “BWANA ni fungu langu, kwa hiyo nitamngojea.” BWANA ni mwema kwa wale wanaomtumaini, na kwa yule anayemtafuta