Maombolezo 3:1-9
Maombolezo 3:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi ni mtu niliyepata mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake Mungu. Amenichukua akanipeleka mpaka gizani kusiko na mwanga. Amenyosha mkono wake dhidi yangu mimi tu, akanichapa tena na tena mchana kutwa. Amenichakaza ngozi na nyama, mifupa yangu ameivunja. Amenizingira na kunizungushia uchungu na mateso. Amenikalisha gizani kama watu waliokufa zamani. Amenizungushia ukuta nisitoroke, amenifunga kwa minyororo mizito. Ingawa naita na kulilia msaada anaizuia sala yangu isimfikie. Njia zangu ameziziba kwa mawe makubwa amevipotosha vichochoro vyangu.
Maombolezo 3:1-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mimi ni mtu aliyeona mateso Kwa fimbo ya ghadhabu yake. Ameniongoza na kunipeleka katika giza Wala si katika nuru. Hakika juu yangu augeuza mkono wake Mara kwa mara mchana wote. Amechakaza ngozi yangu na nyama yangu; Ameivunja mifupa yangu. Amejenga boma juu yangu, Na kunizungusha uchungu na uchovu. Amenikalisha penye giza, Kama watu waliokufa zamani. Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka; Amenifunga kwa mnyororo mzito. Naam, nikilia na kuomba msaada, Huyapinga maombi yangu. Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa; Ameyapotosha mapito yangu.
Maombolezo 3:1-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mimi ni mtu aliyeona mateso Kwa fimbo ya ghadhabu yake. Ameniongoza na kuniendesha katika giza Wala si katika nuru. Hakika juu yangu augeuza mkono wake Mara kwa mara mchana wote. Amechakaza nyama yangu na ngozi yangu; Ameivunja mifupa yangu. Amejenga boma juu yangu, Na kunizungusha uchungu na uchovu. Amenikalisha penye giza, Kama watu waliokufa zamani. Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka; Ameufanya mnyororo wangu mzito. Naam, nikilia na kuomba msaada, Huyapinga maombi yangu. Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa; Ameyapotosha mapito yangu.
Maombolezo 3:1-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mimi ndiye mtu aliyeona mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake. Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee gizani wala si katika nuru; hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu tena na tena, mchana kutwa. Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa na ameivunja mifupa yangu. Amenizingira na kunizunguka kwa uchungu na taabu. Amenifanya niishi gizani kama wale waliokufa. Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka, amenifunga kwa minyororo mizito. Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada, anakataa kupokea maombi yangu. Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe, amepotosha njia zangu.