Maombolezo 2:20-21
Maombolezo 2:20-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Tazama ee Mwenyezi-Mungu uone! Je, kuna yeyote uliyemtendea ulivyotutendea sisi? Je, hata kina mama wawale watoto wao? Je, nao makuhani wauawe hekaluni mwako? Maiti za vijana na wazee zimelala vumbini barabarani, wasichana na wavulana wangu wameuawa kwa upanga; umewaua bila huruma siku ya hasira yako.
Maombolezo 2:20-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana? Kijana na mzee hulala chini Katika njia kuu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wameanguka kwa upanga; Umewaua katika siku ya hasira yako; Umeua, wala hukuona huruma.
Maombolezo 2:20-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana? Kijana na mzee hulala chini Katika njia kuu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wameanguka kwa upanga; Umewaua katika siku ya hasira yako; Umeua, wala hukuona huruma.
Maombolezo 2:20-21 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Tazama, Ee BWANA, ufikirie: Ni nani ambaye umepata kumtendea namna hii? Je, wanawake wale wazao wao, watoto waliowalea? Je, kuhani na nabii auawe mahali patakatifu pa Bwana? “Vijana na wazee hujilaza pamoja katika mavumbi ya barabarani, wasichana wangu na wavulana wangu wameanguka kwa upanga. Umewaua katika siku ya hasira yako, umewachinja bila huruma.