Maombolezo 1:1-5
Maombolezo 1:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Ajabu mji uliokuwa umejaa watu, sasa wenyewe umebaki tupu! Ulikuwa maarufu kati ya mataifa; sasa umekuwa kama mama mjane. Miongoni mwa miji ulikuwa kama binti mfalme; sasa umekuwa mtumwa wa wengine. Walia usiku kucha; machozi yautiririka. Hakuna hata mmoja wa wapenzi wake wa kuufariji. Rafiki zake wote wameuhadaa; wote wamekuwa adui zake. Watu wa Yuda wamekwenda uhamishoni pamoja na mateso na utumwa mkali. Sasa wanakaa miongoni mwa watu wa mataifa, wala hawapati mahali pa kupumzika. Waliowafuatia wamewakamata wakiwa taabuni. Barabara za kwenda Siyoni zinasikitisha; hakuna wapitao kwenda kwenye sikukuu. Malango ya mji wa Siyoni ni tupu; makuhani wake wanapiga kite, wasichana wake wana huzuni, na mji wenyewe uko taabuni. Adui zake ndio wanaoutawala na wanafanikiwa, kwani Mwenyezi-Mungu ameutesa kwa sababu ya makosa mengi. Watoto wake wametekwa na kupelekwa mbali.
Maombolezo 1:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa! Hulia sana wakati wa usiku, Na machozi yake yapo mashavuni; Miongoni mwa wote waliompenda Hakuna hata mmoja amfarijiye; Rafiki zake wote wamemtenda hila, Wamekuwa adui zake. Yuda amehamishwa kwa sababu ya kuonewa, Na kwa sababu ya utumwa mkuu; Anakaa kati ya mataifa, Haoni raha yoyote; Wote waliomfuata wamempata Katika dhiki yake. Njia za Sayuni zaomboleza, Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu; Malango yake yote yamekuwa ukiwa, Makuhani wake hupiga kite; Wanawali wake wanahuzunika; Na yeye mwenyewe huona uchungu. Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa BWANA amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi.
Maombolezo 1:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa! Hulia sana wakati wa usiku, Na machozi yake yapo mashavuni; Miongoni mwa wote waliompenda Hakuna hata mmoja amfarijiye; Rafiki zake wote wamemtenda hila, Wamekuwa adui zake. Yuda amehamishwa kwa sababu ya kuonewa, Na kwa sababu ya utumwa mkuu; Anakaa kati ya makafiri, Haoni raha iwayo yote; Wote waliomfuata wamempata Katika dhiki yake. Njia za Sayuni zaomboleza, Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu; Malango yake yote yamekuwa ukiwa, Makuhani wake hupiga kite; Wanawali wake wanahuzunika; Na yeye mwenyewe huona uchungu. Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa BWANA amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi.
Maombolezo 1:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Tazama jinsi mji ulivyoachwa ukiwa, mji ambao zamani ulikuwa umejaa watu! Jinsi umekuwa kama mama mjane, ambaye wakati fulani alikuwa maarufu miongoni mwa mataifa! Yule aliyekuwa malkia miongoni mwa majimbo sasa amekuwa mtumwa. Kwa uchungu, hulia sana usiku, machozi yapo kwenye mashavu yake. Miongoni mwa wapenzi wake wote hakuna yeyote wa kumfariji. Rafiki zake wote wamemsaliti, wamekuwa adui zake. Baada ya mateso na kufanyishwa kazi kikatili, Yuda ameenda uhamishoni. Anakaa miongoni mwa mataifa, hapati mahali pa kupumzika. Wote ambao wanamsaka wamemkamata katikati ya dhiki yake. Barabara zielekeazo Sayuni zaomboleza, kwa kuwa hakuna yeyote anayekuja kwenye sikukuu zake zilizoamriwa. Malango yake yote yamekuwa ukiwa, makuhani wake wanalia kwa uchungu, wanawali wake wanahuzunika, naye yuko katika uchungu wa maumivu makuu. Adui zake wamekuwa mabwana zake, watesi wake wana amani. BWANA amemletea huzuni kwa sababu ya dhambi zake nyingi. Watoto wake wameenda uhamishoni, wamekuwa mateka mbele ya adui.