Maombolezo 1:1
Maombolezo 1:1 Biblia Habari Njema (BHN)
Ajabu mji uliokuwa umejaa watu, sasa wenyewe umebaki tupu! Ulikuwa maarufu kati ya mataifa; sasa umekuwa kama mama mjane. Miongoni mwa miji ulikuwa kama binti mfalme; sasa umekuwa mtumwa wa wengine.
Maombolezo 1:1 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa!
Maombolezo 1:1 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa!
Maombolezo 1:1 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Tazama jinsi mji ulivyoachwa ukiwa, mji ambao zamani ulikuwa umejaa watu! Jinsi umekuwa kama mama mjane, ambaye wakati fulani alikuwa maarufu miongoni mwa mataifa! Yule aliyekuwa malkia miongoni mwa majimbo sasa amekuwa mtumwa.