Yuda 1:17-21
Yuda 1:17-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini nyinyi wapenzi wangu, kumbukeni yale mliyoambiwa hapo awali na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo. Waliwaambieni: “Siku za mwisho, watatokea watu watakaowadhihaki nyinyi, watu wafuatao tamaa zao mbaya.” Hao ndio wanaosababisha mafarakano, watu wa fikira za kidunia, wasio na Roho wa Mungu. Lakini nyinyi, wapenzi wangu, jijengeni wenyewe juu ya imani yenu takatifu kabisa. Salini kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, na kudumu katika upendo wa Mungu, mkimngojea Bwana wetu Yesu Kristo ambaye, kwa huruma yake, atawajalieni uhai wa milele.
Yuda 1:17-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo, ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa za upotevu wao wenyewe. Watu hao ndio waletao utengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho. Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu, jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.
Yuda 1:17-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo, ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu. Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho. Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu, jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.
Yuda 1:17-21 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini ninyi wapendwa, kumbukeni yale mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo waliyotabiri awali. Kwa kuwa waliwaambia, “Siku za mwisho kutakuwa na watu wenye kudhihaki, watakaofuata tamaa zao wenyewe za upotovu.” Hawa ndio watu wanaowagawanya ninyi, wanaofuata tamaa zao za asili, wala hawana Roho. Lakini ninyi wapendwa, jijengeni katika imani yenu iliyo takatifu sana tena ombeni katika Roho Mtakatifu. Jilindeni katika upendo wa Mungu mkitazamia rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, inayowapeleka katika uzima wa milele.