Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 7:16-18 - Compare All Versions

Yoshua 7:16-18 BHN (Biblia Habari Njema)

Basi, Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawaleta Waisraeli wote karibu, kabila baada ya kabila; kabila la Yuda likachaguliwa. Akazileta karibu koo za Yuda, ukoo baada ya ukoo; na ukoo wa Zerahi ukachaguliwa. Akazileta karibu jamaa za ukoo wa Zerahi, jamaa baada ya jamaa; na jamaa ya Zabdi ikachaguliwa. Yoshua akaileta jamaa ya Zabdi karibu, nyumba baada ya nyumba; na nyumba ya Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, ikachaguliwa.

Shirikisha
Yoshua 7 BHN

Yoshua 7:16-18 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Basi Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, akawasongeza Israeli kabila kwa kabila; kabila la Yuda likatwaliwa. Akazisongeza jamaa za Yuda, akaitwaa jamaa ya Wazera; akaisongeza jamaa ya Wazera mtu kwa mtu; Zabdi akatwaliwa. Akawasongeza watu wa nyumba yake mmoja mmoja; na Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda akatwaliwa.

Shirikisha
Yoshua 7 SRUV

Yoshua 7:16-18 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Basi Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, akawasogeza Israeli kabila kwa kabila; kabila ya Yuda ikatwaliwa. Akazisogeza jamaa za Yuda, akaitwaa jamaa ya Wazera; akaisogeza jamaa ya Wazera mtu kwa mtu; Zabdi akatwaliwa. Akawasogeza watu wa nyumba yake mmoja mmoja; na Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda akatwaliwa.

Shirikisha
Yoshua 7 SUV

Yoshua 7:16-18 NEN (Neno)

Kesho yake asubuhi na mapema Yoshua akaamuru Israeli kuja mbele kabila kwa kabila; na kabila la Yuda likachaguliwa. Koo za Yuda zikaja mbele, naye akawachagua Wazera. Akaamuru ukoo wa Wazera kuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa ya Zabdi ikachaguliwa. Yoshua akaamuru jamaa ya Zabdi kuja mbele mtu kwa mtu, naye Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, akachaguliwa.

Shirikisha
Yoshua 7 NEN