Yoshua 7:1
Yoshua 7:1 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini Waisraeli hawakuwa waaminifu kuhusu vile vitu vilivyotolewa viangamizwe kwani Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, alichukua baadhi ya vitu vilivyoamriwa viteketezwe. Kwa hiyo hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawaka dhidi ya Waisraeli.
Yoshua 7:1 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini Waisraeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya BWANA ikawaka juu ya Waisraeli.
Yoshua 7:1 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya BWANA ikawaka juu ya wana wa Israeli.
Yoshua 7:1 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini Waisraeli hawakuwa waaminifu kuhusu vile vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa; Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, alivichukua baadhi ya hivyo vitu. Hasira ya BWANA ikawaka dhidi ya Israeli.