Yoshua 3:5-6
Yoshua 3:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Yoshua akawaambia watu, “Jitakaseni kwa kuwa kesho Mwenyezi-Mungu atatenda maajabu kati yenu.” Kisha akawaambia makuhani, “Chukueni sanduku la agano, mtangulie nalo mbele ya watu.” Nao wakalichukua na kutangulia mbele ya watu.
Yoshua 3:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yoshua akawaambia watu, Jitakaseni; maana kesho BWANA atatenda mambo ya ajabu kati yenu. Kisha Yoshua akawaambia makuhani, akasema, Liinueni sanduku la Agano, mkavuke mbele ya hao watu. Wakaliinua sanduku la Agano, wakatangulia mbele ya watu.
Yoshua 3:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yoshua akawaambia watu, Jitakaseni; maana kesho BWANA atatenda mambo ya ajabu kati yenu. Kisha Yoshua akawaambia makuhani, akasema, Liinueni sanduku la agano, mkavuke mbele ya hao watu. Wakaliinua sanduku la agano, wakatangulia mbele ya watu.
Yoshua 3:5-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo Yoshua akawaambia hao watu, “Jitakaseni, kwa kuwa kesho BWANA atatenda mambo ya kushangaza kati yenu.” Yoshua akawaambia makuhani, “Liinueni Sanduku la Agano mkatangulie mbele ya watu.” Hivyo wakaliinua na kutangulia mbele yao.