Yoshua 24:22-24
Yoshua 24:22-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Hapo Yoshua akawaambia, “Nyinyi wenyewe ni mashahidi wa nafsi zenu kwamba mmechagua kumtumikia Mwenyezi-Mungu.” Nao wakamjibu, “Sisi tu mashahidi.” Naye akawaambia, “Basi, ondoeni miungu ya kigeni mliyo nayo, mkamfuate Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kwa moyo wenu wote.” Nao, wakasema, “Tutamtumikia na kumtii Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.”
Yoshua 24:22-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yoshua akawaambia watu, Ninyi mmekuwa mashahidi juu ya nafsi zenu, ya kuwa mmemchagua BWANA, ili kumtumikia yeye. Wakasema, Sisi tu mashahidi. Akasema, Basi sasa, iondoeni miungu migeni iliyo kati yenu, mkaielekeze mioyo yenu kwa BWANA, Mungu wa Israeli. Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, BWANA, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii.
Yoshua 24:22-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yoshua akawaambia watu, Ninyi mmekuwa mashahidi juu ya nafsi zenu, ya kuwa mmemchagua BWANA, ili kumtumikia yeye. Wakasema, Sisi tu mashahidi. Akasema, Basi sasa, iondoeni miungu migeni iliyo kati yenu, mkaielekeze mioyo yenu kwa BWANA, Mungu wa Israeli. Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, BWANA, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii.
Yoshua 24:22-24 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo Yoshua akawaambia, “Ninyi mmekuwa mashahidi juu yenu wenyewe kuwa mmechagua kumtumikia BWANA.” Nao wakajibu, “Ndiyo, tu mashahidi.” Yoshua akawaambia, “Sasa basi, itupeni mbali hiyo miungu migeni mliyo nayo, nanyi mtoleeni BWANA, Mungu wa Israeli, mioyo yenu.” Nao watu wakamwambia Yoshua, “Tutamtumikia BWANA Mungu wetu na kumtii yeye.”