Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 19:1-51

Yoshua 19:1-51 Biblia Habari Njema (BHN)

Kura ya pili ilizipata koo za kabila la Simeoni na sehemu yao ya nchi ilikuwa imezungukwa na ile ya kabila la Yuda. Kabila la Simeoni lilipata miji ya Beer-sheba, Sheba, Molada Hasar-shuali, Bala, Esemu, Eltoladi, Bethuli, Horma, Siklagi, Beth-markabothi, Hasar-susa, Beth-lebaothi na Sharuheni. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake. Pia kulikuwa na miji ya En-rimoni, Etheri, na Ashani. Jumla ya miji waliyopewa ni minne pamoja na vijiji vyake. Pamoja na vijiji vyote vilivyoizunguka miji hiyo hadi Baalath-beeri, (au Rama) ya Negebu. Hizo zote ni sehemu zilizopewa koo za kabila la Simeoni. Kwa vile eneo lililopewa kabila la Yuda lilikuwa kubwa kuliko kabila hilo lilivyohitaji, sehemu ya eneo lake lilipewa kabila la Simeoni. Kura ya tatu ilizipata koo za kabila la Zebuluni. Eneo lao lilienea hadi Saridi. Kutoka huko mpaka wake ulikwenda magharibi hadi Mareali, ukapitia pembeni mwa Dabeshethi na kwenda kwenye kijito kilichoko mashariki ya Yokneamu. Kutoka Saridi, mpaka huo ulielekea mashariki hadi kwenye mpaka wa Kisloth-tabori, na kutoka huko ukapita Daberathi hadi Yafia. Kutoka Yafia uliendelea mashariki hadi Gath-heferi, Eth-kasini, na kuendelea hadi Rimoni ambako ulipanda kuelekea Nea. Upande wa kaskazini mpaka uligeuka kuelekea Hanathoni na kuishia kwenye bonde la Yiftaheli. Ukajumuisha miji ya Katathi, Nahalali, Shimroni, Yidala na Bethlehemu. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na miwili pamoja na vijiji vyake. Hiyo ndiyo sehemu zilizopewa koo za kabila la Zebuluni miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Kura ya nne ilizipata koo za kabila la Isakari. Eneo lenyewe lilikuwa na miji ya Yezreeli, Kesulothi, Shunemu, Hafaraimu, Shioni, Anaharathi, Rabithi, Kishioni, Ebesi, Remethi, En-ganimu, En-hada na Beth-pasesi. Kadhalika, mpaka wao ulifika Tabori, Shahasuma, Beth-shemeshi na kuishia kwenye mto Yordani. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na sita pamoja na vijiji vyake. Hizo ndizo sehemu zilizopewa koo za kabila la Isakari; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Kura ya tano ilizipata koo za kabila la Asheri. Eneo la nchi yao lilikuwa na miji ya Helkathi, Hali, Beteni, Akshafi, Alameleki, Amadi na Mishali. Kwa upande wa magharibi mpaka uligusana na Karmeli na Shihor-libnathi. Kisha ukageuka kuelekea mashariki kwenda Beth-dagoni ambako unagusana na Zebuluni na bonde la Iftaheli. Halafu ukaendelea kaskazini hadi Beth-emeki, Neieli na kuzidi kuelekea kaskazini hadi Kabuli, Ebroni, Rehobu, Hamoni, Kana hadi Sidoni Kuu. Hapo, mpaka uligeuka kuelekea Rama na kufikia kwenye mji wa Tiro uliokuwa na ngome. Kisha ukageuka kuelekea Hosa na kuishia kwenye bahari ya Mediteranea. Miji mingine iliyokuwamo ni Maharabu, Akzibu, Uma, Afeka na Rehobu. Jumla ya miji waliyopewa ni ishirini na miwili pamoja na vijiji vyake. Sehemu hizo ndizo zilizopewa koo za kabila la Asheri; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Kura ya sita ilizipata koo za kabila la Naftali. Mpaka wake ulianzia Helefu na mwaloni mwa Zaananimu, ukapita Adami-nekebu na Yabneeli hadi Lakumu na kuishia kwenye mto Yordani. Kutoka hapo mpaka ulikwenda magharibi kuelekea Aznoth-tabori; toka huko ukaenda Hukoki na kugusana na pembe ya kusini ya eneo la kabila la Zebuluni; kisha kugusana na eneo la kabila la Asheri upande wa magharibi, na kugusana na eneo la kabila la Yuda. Kwa upande wa mashariki mpaka ukiingilia kwenye mto Yordani. Miji yao iliyokuwa na ngome ni Zidimu, Zeri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi, Adama, Rama, Hazori, Kedeshi, Edrei, En-hazori, Yironi, Migdaleli, Horemu, Beth-anathi na Beth-shemeshi. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na tisa pamoja na vijiji vyake. Hizo ndizo sehemu zilizopewa koo za kabila la Naftali; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Kura ya saba ilizipata koo za kabila la Dani. Eneo la nchi yao lilikuwa na miji ya Sora, Eshtaoli, Ir-shemeshi Shaalabini, Aiyaloni, Yithla, Eloni, Timna, Ekroni Elteke, Gibethoni, Baalathi, Yehudi, Bene-beraki, Gath-rimoni, Me-yarkoni na Rakoni na nchi iliyokuwa karibu na Yopa. Watu wa kabila la Dani walipopoteza nchi yao, walikwenda na kuushambulia mji wa Leshemu. Waliushinda na kuuteka, na baada ya kuwaua wakazi wake wote, waliumiliki halafu wakabadili jina la mji huo kuwa Dani; jina ambalo lilikuwa ni la babu yao. Hizo ndizo sehemu zilizopewa koo za kabila la Dani; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Walipomaliza kugawiana sehemu zote za nchi, Waisraeli walimpa Yoshua, mwana wa Nuni, sehemu yake katikati yao. Kulingana na amri ya Mwenyezi-Mungu walimpa mji ambao aliuchagua yeye mwenyewe, yaani Timnath-sera, ambao ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu. Naye Yoshua akaujenga upya mji huo na kukaa humo. Basi, kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, pamoja na viongozi wa makabila ya Waisraeli waligawa sehemu hizo kwa kura mbele ya Mwenyezi-Mungu mlangoni mwa hema la mkutano huko Shilo. Basi, wakakamilisha kuigawa nchi.

Shirikisha
Soma Yoshua 19

Yoshua 19:1-51 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Kisha sehemu ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hilo kabila la wana wa Simeoni, kwa kufuata jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda. Miji waliyokuwa nayo katika urithi wao ni Beer-sheba, Sheba, Molada; Hasar-shuali, Bala, Esemu; Eltoladi, Bethuli, Horma; Siklagi, Beth-markabothi, Hasarsusa; Bethlebaothi na Sharuheni; miji kumi na mitatu, pamoja na vijiji vyake; Aini, Rimoni, Etheri na Ashani; miji minne, pamoja na vijiji vyake; tena vijiji vyote vilivyozunguka miji hiyo kotekote mpaka Baalath-beeri, Rama wa Kusini. Huo ndio urithi wa kabila la wana wa Simeoni kwa kuandama jamaa zao. Huo urithi wa hao wana wa Simeoni ulitoka katika fungu la wana wa Yuda; kwa maana hilo fungu la wana wa Yuda lilikuwa ni kubwa mno kwao; kwa hiyo wana wa Simeoni walikuwa na urithi katikati ya urithi wao. Kisha sehemu ya tatu ilitokea kwa ajili ya wana wa Zabuloni kwa kufuata jamaa zao; na mpaka wa urithi wao ulifikia hadi Saridi; kisha mpaka wao ukakwea kwendelea upande wa magharibi, hadi kufikia Marala, nao ukafikia hadi Dabeshethi; nao ukafikia kijito cha maji kilicho mkabala wa Yokneamu; kisha ukazunguka kutoka Saridi kwendelea upande wa mashariki kwa kuelekea maawio ya jua hata kufikia mpaka wa Kisiloth-ubori; kisha ukatokea hata Daberathi, kisha ukakwea kwendelea Yafia; kutoka hapo ukaendelea kuelekea mashariki mpaka Gath-heferi, hadi kufikia Ethkasini; kisha ukatokea huko Rimoni ufikialo hadi Nea; kisha mpaka uliizunguka nchi hiyo kwa upande wa kaskazini hadi Hanathoni; kisha mwisho wake ulikuwa katika bonde la Iftaeli; Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake. Huu ndio urithi wa wana wa Zabuloni kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake. Kisha sehemu ya nne ilitokea kwa ajili ya Isakari, maana, ni kwa ajili ya wana wa Isakari kwa kufuata jamaa zao. Na mpaka wao ulifikia Yezreeli, Kesulothi, Shunemu; Hafaraimu, Shioni, Anaharathi; Rabithu, Kishioni, Ebesi; Remethi, Enganimu, Enhada, Bethpasesi; na mpaka ukafikia hadi Tabori, na Shahasuma na Beth-shemeshi; na mwisho wa mpaka wao ulikuwa katika mto wa Yordani; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake. Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Isakari kwa kufuata jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Kisha sehemu ya tano ilitokea kwa ajili ya kabila la wana wa Asheri kwa kufuata jamaa zao. Na mpaka wao ulikuwa ni Helkathi, Hali, Beteni, Akishafu; Alameleki, Amadi na Mishali; nao ukafika hadi Karmeli upande wa magharibi, tena ulifikia hadi Shihor-libnathi; kisha ukazunguka kuelekea maawio ya jua mpaka Beth-dagoni, nao ukafikia hadi Zabuloni, tena mpaka bonde la Iftaeli upande wa kaskazini hadi Bethemeki na Neyeli; kisha ukatokea hadi Kabuli upande wa kushoto; na Ebroni, Rehobu, Hamoni, Kana, hadi kufikia Sidoni Kuu; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu; na Uma pia, na Afeka, na Rehobu; miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake. Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Asheri kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake. Kisha sehemu ya sita ikatokea kwa ajili ya wana wa Naftali, maana, ni kwa ajili ya wana wa Naftali kwa kufuata jamaa zao. Na mpaka wao ulikuwa kutoka Helefu, tokea ule mwaloni ulio katika Saananimu, na Adami-nekebu, na Yabneeli, hadi kufikia Lakumu; na matokeo yake yalikuwa katika mto wa Yordani; tena mpaka ulizunguka kwendelea upande wa magharibi hadi Aznoth-tabori, tena kutoka hapo ukaendelea mpaka Hukoki; kisha ukafikia hadi Zabuloni upande wa kusini, tena ulifikia hadi Asheri upande wa magharibi, tena ulifikia hata Yuda hapo katika mto wa Yordani kwa upande wa kuelekea maawio ya jua. Na miji yenye boma ilikuwa ni hii, Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi; Adama, Rama Hazori; Kedeshi, Edrei, Enhasori; Ironi, Migdal-eli, Horemu, Bethanathi na Beth-shemeshi; miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake. Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Naftali kwa kufuata jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Kisha sehemu ya saba ilitokea kwa ajili ya kabila la wana wa Dani kwa kufuata jamaa zao. Na mpaka wa urithi wao ulikuwa ni Sora, Eshtaoli, Irishemeshi; Shaalabini, Aiyaloni, Ithla; Eloni, Timna, Ekroni; Elteka, Gibethoni, Baalathi; Yehudi, Bene-beraki, Gath-rimoni; Meyarkoni na Rakoni, pamoja na huo mpaka uliokuwa mkabala wa Yafa. Kisha mpaka wa wana wa Dani ulitokea kuwapita wao; kwa kuwa hao wana wa Dani wakakwea na kupigana na Leshemu, na kuutwaa, na kuupiga kwa makali ya upanga, na kuumiliki, nao wakakaa humo, wakauita Dani, kwa kuliandama jina la huyo Dani mzee wao. Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Dani kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake. Basi walipomaliza kazi yao hiyo ya kuigawanya nchi iwe urithi kwa kufuata mipaka yake; wana wa Israeli kakampa Yoshua, mwana wa Nuni, urithi katikati yao; kulingana na ile amri ya BWANA wakampa mji alioutaka, maana, ni Timnath-sera katika nchi ya vilima ya Efraimu; naye akaujenga huo mji na kukaa mumo. Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa ya makabila ya Waisraeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele ya BWANA, hapo mlangoni mwa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.

Shirikisha
Soma Yoshua 19

Yoshua 19:1-51 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Kisha kura ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hiyo kabila ya wana wa Simeoni, kwa kuandama jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda. Miji waliyokuwa nayo katika urithi wao ni Beer-sheba, na Sheba, na Molada; na Hasarshuali, na Bala, na Esemu; na Eltoladi, na Bethuli, na Horma; na Siklagi, na Bethmarkabothi, na Hasarsusa; na Bethlebaothi, na Sharuheni; miji kumi na mitatu, pamoja na vijiji vyake; na Aini, na Rimoni, na Etheri, na Ashani; miji minne, pamoja na vijiji vyake; tena vijiji vyote vilivyozunguka miji hiyo kote kote mpaka Baalath-beeri, Rama wa Kusini. Huo ndio urithi wa kabila ya wana wa Simeoni kwa kuandama jamaa zao. Huo urithi wa hao wana wa Simeoni ulitoka katika fungu la wana wa Yuda; kwa maana hilo fungu la wana wa Yuda lilikuwa ni kubwa mno kwao; kwa hiyo wana wa Simeoni walikuwa na urithi katikati ya urithi wao. Kisha kura ya tatu ilitokea kwa ajili ya wana wa Zabuloni kwa kuandama jamaa zao; na mpaka wa urithi wao ulifikilia hata Saridi; kisha mpaka wao ukakwea kwendelea upande wa magharibi, hata kufikilia Marala, nao ukafikilia hata Dabeshethi; nao ukafikilia kijito cha maji kilicho mkabala wa Yokneamu; kisha ukazunguka kutoka Saridi kwendelea upande wa mashariki kwa kuelekea maawio ya jua hata kufikilia mpaka wa Kisiloth-ubori; kisha ukatokea hata Daberathi, kisha ukakwea kwendelea Yafia; kutoka hapo ukaendelea kuelekea mashariki mpaka Gath-heferi, hata kufikilia Ethkasini; kisha ukatokea huko Rimoni ufikiliao hata Nea; kisha mpaka uliizunguka nchi hiyo kwa upande wa kaskazini hata Hanathoni; kisha matokeo yake yalikuwa katika bonde la Iftaeli; na Katathi, na Nahalali, na Shimroni, na Idala, na Bethlehemu; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake. Huu ndio urithi wa wana wa Zabuloni kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake. Kisha kura ya nne ilitokea kwa ajili ya Isakari, maana, ni kwa ajili ya wana wa Isakari kwa kuandama jamaa zao. Na mpaka wao ulifikilia Yezreeli, na Kesulothi, na Shunemu; na Hafaraimu, na Shioni, na Anaharathi; na Rabithu, na Kishioni, na Ebesi; na Remethi, na Enganimu, na Enhada, na Bethpasesi; na mpaka ukafikilia hata Tabori, na Shahasuma na Bethshemeshi; na matokeo ya mpaka wao yalikuwa katika mto wa Yordani; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake. Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Isakari kwa kuandama jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Kisha kura ya tano ilitokea kwa ajili ya kabila ya wana wa Asheri kwa kuandama jamaa zao. Na mpaka wao ulikuwa ni Helkathi, na Hali, na Beteni, na Akishafu; na Alameleki, na Amadi, na Mishali; nao ukafikilia hata Karmeli upande wa magharibi, tena ulifikilia hata Shihor-libnathi; kisha ukazunguka kuelekea maawio ya jua mpaka Beth-dagoni, nao ukafikilia hata Zabuloni, tena mpaka bonde la Iftaeli upande wa kaskazini hata Bethemeki na Neyeli; kisha ukatokea hata Kabuli upande wa kushoto; na Ebroni, na Rehobu, na Hamoni, na Kana, hata kufikilia Sidoni mkuu; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu; na Uma pia, na Afeka, na Rehobu; miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake. Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Asheri kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake. Kisha kura ya sita ikatokea kwa ajili ya wana wa Naftali, maana, ni kwa ajili ya wana wa Naftali kwa kuandama jamaa zao. Na mpaka wao ulikuwa kutoka Helefu, tokea ule mwaloni ulio katika Saananimu, na Adami-nekebu, na Yabineeli, hata kufikilia Lakumu; na matokeo yake yalikuwa katika mto wa Yordani; tena mpaka ulizunguka kwendelea upande wa magharibi hata Aznoth-tabori, tena kutoka hapo ukaendelea mpaka Hukoki; kisha ukafikilia hata Zabuloni upande wa kusini, tena ulifikilia hata Asheri upande wa magharibi, tena ulifikilia hata Yuda hapo katika mto wa Yordani kwa upande wa kuelekea maawio ya jua. Na miji yenye boma ilikuwa ni hii, Sidimu, na Seri, na Hamathi, na Rakathi, na Kinerethi; na Adama, na Rama, na Hazori; na Kedeshi, na Edrei, na Enhasori; na Ironi, na Migdal-eli, na Horemu, na Bethanathi, na Bethshemeshi; miji kumi na kenda, pamoja na vijiji vyake. Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Naftali kwa kuandama jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Kisha kura ya saba ilitokea kwa ajili ya kabila ya wana wa Dani kwa kuandama jamaa zao. Na mpaka wa urithi wao ulikuwa ni Sora, na Eshtaoli, na Irishemeshi; na Shaalabini, na Aiyaloni, na Ithla; na Eloni, na Timna, na Ekroni; na Elteka, na Gibethoni, na Baalathi; na Yehudi, na Bene-beraki, na Gathrimoni; na Meyarkoni, na Rakoni, pamoja na huo mpaka uliokuwa mkabala wa Yafa. Kisha mpaka wa wana wa Dani ulitokea kuwapita wao; kwa kuwa hao wana wa Dani wakakwea na kupigana na Leshemu, na kuutwaa, na kuupiga kwa makali ya upanga, na kuumiliki, nao wakakaa humo, wakauita Dani, kwa kuliandama jina la huyo Dani mzee wao. Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Dani kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake. Basi wakamaliza hiyo kazi yao ya kuigawanya nchi iwe urithi kwa kuandama mipaka yake; kisha wana wa Israeli wakampa Yoshua, mwana wa Nuni, urithi katikati yao; sawasawa na ile amri ya BWANA wakampa mji alioutaka, maana, ni Timnath-sera katika nchi ya vilima ya Efraimu; naye akaujenga huo mji na kukaa mumo. Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa ya kabila za wana wa Israeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele ya BWANA, hapo mlangoni mwa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.

Shirikisha
Soma Yoshua 19

Yoshua 19:1-51 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, kufuatana na koo zao. Urithi wao ulikuwa ndani ya eneo la Yuda. Ulijumuisha: Beer-Sheba (au Sheba), Molada, Hasar-Shuali, Bala, Esemu, Eltoladi, Bethuli, Horma, Siklagi, Beth-Markabothi, Hasar-Susa, Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na tatu pamoja na vijiji vyake. Pia Aini, Rimoni, Etheri, na Ashani; hii ilikuwa miji minne na vijiji vyake, pamoja na vijiji vyote vinavyoizunguka miji hii hadi Baalath-Beeri (ambayo ndiyo Rama iliyo katika Negebu). Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simeoni kufuatana na koo zao. Urithi wa Wasimeoni ulitolewa kutoka fungu la Yuda, kwa kuwa fungu la Yuda lilikuwa kubwa kuliko walivyohitaji. Hivyo kabila la Simeoni lilipewa urithi wao ndani ya eneo la Yuda. Kura ya tatu ikaangukia kabila la Zabuloni, kufuatana na koo zao: Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi. Kuelekea upande wa magharibi ukafika Marala, ukagusa Dabeshethi, na kuendelea hadi kwenye bonde karibu na Yokneamu. Ukageuka mashariki, kuanzia Saridi kuelekea mawio ya jua hadi kwenye nchi ya Kisiloth-Tabori, na kwenda hadi Daberathi, kupanda Yafia. Kisha ukaendelea mashariki hadi Gath-Heferi na kufika Eth-Kasini, ukatokea Rimoni na kugeuka kuelekea Nea. Huko mpaka ukazungukia upande wa kaskazini hadi Hanathoni na kuishia katika Bonde la Ifta-Eli. Miji mingine iliyojumuishwa ni Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na mbili pamoja na vijiji vyake. Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa Zabuloni, kufuatana na koo zao. Kura ya nne ikaangukia kabila la Isakari, kufuatana na koo zao. Eneo lao lilijumuisha: Yezreeli, Kesulothi, Shunemu, Hafaraimu, Shioni, Anaharathi, Rabithi, Kishioni, Ebesi, Remethi, En-Ganimu, En-Hada na Beth-Pasesi. Mpaka ule ukagusa Tabori, Shahasuma na Beth-Shemeshi, na ukaishia kwenye Yordani. Ilikuwa miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake. Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Isakari, kufuatana na koo zao. Kura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, kufuatana na koo zao. Eneo lao lilijumuisha: Helkathi, Hali, Beteni, Akshafu, Alameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi. Tena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto. Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu. Mpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika eneo la Akzibu, Uma, Afeki na Rehobu. Ilikuwa miji ishirini na mbili, pamoja na vijiji vyake. Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Asheri, kufuatana na koo zao. Kura ya sita ikaangukia kabila la Naftali, kufuatana na koo zao: Mpaka wao uliendelea kutoka Helefi na kwenye mwaloni ulio Saananimu, ukipitia Adami-Nekebu na Yabineeli hadi Lakumu, na kuishia katika Mto Yordani. Mpaka ukaendelea magharibi kupitia Aznoth-Tabori na kutokea Hukoki. Ukagusa Zabuloni upande wa kusini, Asheri upande wa magharibi, na Yordani upande wa mashariki. Miji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi, Adama, Rama, Hazori, Kedeshi, Edrei, na En-Hasori, Ironi, Migdal-Eli, Horemu, Beth-Anathi na Beth-Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa na vijiji vyake. Miji hiyo pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Naftali, kufuatana na koo zao. Kura ya saba ikaangukia kabila la Dani, kufuatana na koo zao. Eneo la urithi wao lilijumuisha: Sora, Eshtaoli, Iri-Shemeshi, Shaalabini, Aiyaloni, Ithla, Eloni, Timna, Ekroni, Elteke, Gibethoni, Baalathi, Yehudi, Bene-Beraki, Gath-Rimoni, Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa. (Lakini Wadani walipata shida kulimiliki eneo lao; kwa hiyo walipanda kuishambulia Leshemu, wakaitwaa, wakawaua watu wake kwa upanga na kuukalia. Walikaa Leshemu na kuuita Dani kufuatana na jina la baba yao.) Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Dani, kufuatana na koo zao. Walipomaliza kuigawa nchi kulingana na sehemu zilizowaangukia, Waisraeli walimpa Yoshua mwana wa Nuni urithi kati yao, kama vile BWANA alivyokuwa ameamuru. Walimpa mji alioutaka, ambao ni Timnath-Sera ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu. Naye akajenga mji, akakaa huko. Haya ndio maeneo ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za makabila ya Israeli waliyagawanya kwa kura huko Shilo mbele za BWANA, penye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo wakamaliza kuigawanya nchi.

Shirikisha
Soma Yoshua 19