Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 18:11-28

Yoshua 18:11-28 Biblia Habari Njema (BHN)

Kura ya kwanza ililipata kabila la Benyamini kulingana na koo zake. Eneo walilopewa watu hao lilikuwa katikati ya lile la kabila la Yuda na lile la kabila la Yosefu. Mpaka wake wa kaskazini ulianzia mto Yordani na kupitia kaskazini mwa Yeriko na nchi ya milima ukaelekea magharibi hadi kwenye nyika ya Beth-aveni. Kutoka huko, mpaka wake ulikwenda kusini kuelekea Luzu kupitia upande wa kusini wa Luzu (yaani Betheli) hadi Ataroth-adari, kwenye mlima ulioko kusini mwa Beth-horoni ya Chini. Upande wa magharibi wa mlima huo ulio kusini mwa Beth-horoni mpaka uligeuka ukaelekea kusini hadi Kiriath-baali, uitwao pia Kiriath-yearimu, mji ambao ni mali ya kabila la Yuda. Huu ndio uliokuwa mpaka wake upande wa magharibi. Upande wa kusini mpaka wake ulianzia kwenye viunga vya mji wa Kiriath-yearimu, ukafika Efroni na kwenda hadi kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa. Kisha ulielekea chini kupitia pembeni mwa mlima ulioko karibu na bonde la mwana wa Hinomu, ambalo lilikuwa katika sehemu ya kaskazini zaidi ya bonde la Warefai. Halafu mpaka uliteremka kuelekea bonde la Hinomu, kusini mwa kilima cha Wayebusi, ukaendelea kuteremka hadi En-rogeli. Huko, mpaka uligeuka kwenda kaskazini kuelekea En-shemeshi, ukapitia Gelilothi unaokabili mwinuko wa Adumimu na kuteremka hadi kwenye jiwe la Bohani mwana wa Reubeni. Kutoka hapo, mpaka ulizunguka kaskazini kwenye ukingo wa juu wa Araba na kuishia huko Araba. Tena, ukaendelea kwa upande wa kaskazini wa kilima cha Beth-hogla na kuishia kaskazini kabisa ya ghuba ya Bahari ya Chumvi, mahali unapoingilia mto Yordani. Huu ni mpaka wake kwa upande wa kusini. Mto Yordani ndio uliokuwa mpaka wake upande wa mashariki. Ndivyo zilivyowekewa mipaka nchi zilizopewa koo za kabila la Benyamini. Miji ya koo za kabila la Benyamini ni Yeriko, Beth-hogla, Emek-kesisi, Beth-araba, Zemaraimu, Betheli, Avimu, Para, Ofra, Kefar-amoni, Ofni na Geba. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na miwili pamoja na vijiji vyake. Miji mingine ni Gibeoni, Rama, Beerothi, Mizpa, Kefira, Moza, Rekemu, Irpeeli, Tarala, Zela, Ha-elefu, Yebusi, yaani Yerusalemu, Gibea na Kiriath-yearimu. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na minne pamoja na vijiji vyake. Hiyo yote ni sehemu waliyopewa watu wa kabila la Benyamini na koo zao.

Shirikisha
Soma Yoshua 18

Yoshua 18:11-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Kisha ilizuka kura ya kabila la wana wa Benyamini kwa kulingana na jamaa zao; na mpaka wa hiyo kura yao ukatokea kati ya wana wa Yuda na wana wa Yusufu. Mpaka wao upande wa kaskazini ulikuwa kutoka mto wa Yordani; kisha mpaka ukaendelea kufikia ubavuni mwa mji wa Yeriko upande wa kaskazini, kisha ukaendelea kati ya nchi ya vilima kwa kuelekea upande wa magharibi; na matokeo yake yalikuwa hapo penye nyika ya Beth-aveni. Kisha mpaka ukaendelea kutoka hapo na kufikia mji wa Luzu, ubavuni mwa Luzu (ndio Betheli), kwa upande wa kusini; kisha mpaka ukateremkia Ataroth-adari, karibu na mlima ulio upande wa kusini wa Beth-horoni wa chini. Kisha mpaka uliendelea na kuzunguka upande wa magharibi wa kuelekea kusini, kutoka huo mlima ulio mkabala wa Beth-horoni upande wa kusini; na mwisho wake ulikuwa hapo Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), ni mji wa wana wa Yuda; huo ndio upande wa magharibi. Na upande wa kusini ulikuwa ukitoka upande wa mwisho wa Kiriath-yearimu, na mpaka ukatokea upande wa magharibi, ukaendelea hadi chemchemi ya maji, pale Neftoa; kisha mpaka uliteremka hadi mwisho wa mlima ulio pale mkabala wa bonde la mwana wa Hinomu, lililo pale katika bonde la Warefai, upande wa kaskazini; nao ukateremkia mpaka bonde la Hinomu, hadi ubavuni mwa Myebusi upande wa kusini, kisha ukateremka hadi Enrogeli, kisha ulipinda upande wa kaskazini, nao ukatokea hapo Enshemeshi, ukatokea hadi kufikia Gelilothi, ambao ni mkabala wa makweleo ya Adumimu; kisha uliteremka hadi jiwe la Bohani mwana wa Reubeni; kisha ukaendelea mbele ubavuni kuikabili Araba, upande wa kuelekea kaskazini, nao ukateremka hadi hiyo Araba; kisha mpaka ukaendelea mbele ubavuni mwa Beth-hogla upande wa kaskazini; na mwisho wa mpaka ulikuwa katika ile hori ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, mwisho wa kusini wa mto wa Yordani; huo ndio mpaka wa upande wa kusini. Na mto wa Yordani ulikuwa ndio mpaka wake upande wa mashariki. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini, kwa kufuata mipaka yake kwa kuuzunguka kotekote, kulingana na jamaa zao. Basi miji ya kabila la wana wa Benyamini kwa kufuata jamaa zao ilikuwa ni Yeriko, na Beth-hogla, na Emek-kesisi, na Bethiaraba, na Semaraimu, na Betheli; na Avimu, na Para, na Ofra; na Kefar-amoni, na Ofni, na Geba; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake; na Gibeoni, na Rama, na Beerothi; na Mispa, na Kefira, na Moza; na Rekemu, na Irpeeli, na Tarala; na Zela, na Elefu, na huyo Myebusi (ndio Yerusalemu), na Gibeathi, na Kiriathi; miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini kwa kufuata jamaa zao.

Shirikisha
Soma Yoshua 18

Yoshua 18:11-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Kisha ilizuka kura ya kabila ya wana wa Benyamini kwa kuandama jamaa zao; na mpaka wa hiyo kura yao ukatokea kati ya wana wa Yuda na wana wa Yusufu. Mpaka wao upande wa kaskazini ulikuwa kutoka mto wa Yordani; kisha mpaka ukaendelea kufikilia ubavuni mwa mji wa Yeriko upande wa kaskazini, kisha ukaendelea kati ya nchi ya vilima kwa kuelekea upande wa magharibi; na matokeo yake yalikuwa hapo penye nyika ya Bethaveni. Kisha mpaka ukaendelea kutoka hapo na kufikilia mji wa Luzu, ubavuni mwa Luzu (ndio Betheli), kwa upande wa kusini; kisha mpaka ukatelemkia Ataroth-adari, karibu na mlima ulio upande wa kusini wa Beth-horoni wa chini. Kisha mpaka uliendelea na kuzunguka upande wa magharibi wa kuelekea kusini, kutoka huo mlima ulio mkabala wa Beth-horoni upande wa kusini; na matokeo yake yalikuwa hapo Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), ni mji wa wana wa Yuda; huo ndio upande wa magharibi. Na upande wa kusini ulikuwa ukitoka upande wa mwisho wa Kiriath-yearimu, na mpaka ukatokea upande wa magharibi, ukaendelea hata chemchemi ya maji, pale Neftoa; kisha mpaka ulitelemka hata mwisho wa mlima ulio pale mkabala wa bonde la mwana wa Hinomu, lililo pale katika bonde la Warefai, upande wa kaskazini; nao ukatelemkia mpaka bonde la Hinomu, hata ubavuni mwa Myebusi upande wa kusini, kisha ukatelemka hata Enrogeli, kisha ulipigwa upande wa kaskazini, nao ukatokea hapo Enshemeshi, ukatokea hata kufikilia Gelilothi, ambao ni mkabala wa makweleo ya Adumimu; kisha ulitelemka hata jiwe la Bohani mwana wa Reubeni; kisha ukaendelea mbele ubavuni kuikabili Araba, upande wa kuelekea kaskazini, nao ukatelemka hata hiyo Araba; kisha mpaka ukaendelea mbele ubavuni mwa Beth-hogla upande wa kaskazini; na matokeo ya mpaka yalikuwa katika ile hori ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, mwisho wa kusini wa mto wa Yordani; huo ndio mpaka wa upande wa kusini. Na mto wa Yordani ulikuwa ndio mpaka wake upande wa mashariki. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini, kwa kuandama mipaka yake kwa kuuzunguka kote kote, sawasawa na jamaa zao. Basi miji ya kabila ya wana wa Benyamini kwa kuandama jamaa zao ilikuwa ni Yeriko, na Beth-hogla, na Emek-kesisi, na Bethiaraba, na Semaraimu, na Betheli; na Avimu, na Para, na Ofra; na Kefar-amoni, na Ofni, na Geba; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake; na Gibeoni, na Rama, na Beerothi; na Mispa, na Kefira, na Moza; na Rekemu, na Irpeeli, na Tarala; na Zela, na Elefu, na huyo Myebusi (ndio Yerusalemu), na Gibeathi, na Kiriathi; miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini kwa kuandama jamaa zao.

Shirikisha
Soma Yoshua 18

Yoshua 18:11-28 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Kura ya kwanza iliangukia kabila la Benyamini, kufuatana na koo zao. Eneo lao walilogawiwa lilikuwa kati ya kabila la Yuda na la Yusufu. Upande wa kaskazini, mpaka wao ulianzia pale Yordani, kupitia kaskazini mwa mteremko wa Yeriko, na kuendelea magharibi kuingia katika nchi ya vilima, ukitokea kwenye jangwa la Beth-Aveni. Kutoka hapo ulikatiza kwenye mteremko wa kusini mwa Luzu (yaani Betheli) na kushuka hadi Ataroth-Adari katika kilima kusini mwa Beth-Horoni ya Chini. Kutoka kilima kinachotazamana na Beth-Horoni upande wa kusini mpaka ule ukazunguka kusini kufuatia upande wa magharibi, na ukatokezea Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu), mji wa watu wa Yuda. Huu ndio uliokuwa upande wa magharibi. Upande wa kusini mpaka ulianzia kwenye viunga vya Kiriath-Yearimu kwa upande wa magharibi, nao ukatokeza kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa. Mpaka ukateremka hadi shefela inayotazamana na Bonde la Ben-Hinomu, kaskazini mwa Bonde la Warefai. Ukaendelea chini kwenye Bonde la Hinomu sambamba na mteremko wa kusini mwa mji mkubwa wa Wayebusi na kisha hadi En-Rogeli. Kisha ukapinda kuelekea kaskazini, ukaenda hadi En-Shemeshi na kuendelea hadi Gelilothi, inayotazamana na Njia ya Adumimu, ukateremka hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni. Ukaendelea upande wa mteremko wa kaskazini wa Beth-Araba ukateremka hadi Araba. Kisha ukaenda mpaka kwenye mteremko wa kaskazini wa Beth-Hogla na kujitokeza kwenye ghuba ya kaskazini mwa Bahari ya Chumvi, kwenye maingilio ya Yordani upande wa kusini. Huo ulikuwa mpaka wa kusini. Nayo Yordani ikawa ndio mpaka wa upande wa mashariki. Hii ndiyo ilikuwa mipaka iliyoonesha urithi wa koo za Benyamini pande zote. Kabila la Benyamini, kufuatana na koo zao, lilikuwa na miji ifuatayo: Yeriko, Beth-Hogla, Emeki-Kesisi, Beth-Araba, Semaraimu, Betheli, Avimu, Para na Ofra, Kefar-Amoni, Ofni, na Geba; miji kumi na mbili pamoja na vijiji vyake. Gibeoni, Rama na Beerothi, Mispa, Kefira, Moza, Rekemu, Irpeeli, Tarala, Zela, Elefu, mji wa Wayebusi (yaani Yerusalemu), Gibea na Kiriathi; miji kumi na nne, pamoja na vijiji vyake. Huu ndio uliokuwa urithi wa Benyamini kwa ajili ya koo zake.

Shirikisha
Soma Yoshua 18