Yoshua 18:1-3
Yoshua 18:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya kuishinda ile nchi, jumuiya yote ya Waisraeli ilikusanyika huko Shilo na kulisimika hema la mkutano. Yalikuwa yamebaki kati yao makabila saba ambayo hayakuwa yamegawiwa sehemu yao ya nchi. Kwa hiyo, Yoshua akawaambia Waisraeli, “Je, mtakawia mpaka lini kwenda kuimiliki nchi ile ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, amewapeni?
Yoshua 18:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha mkutano mzima wa wana wa Israeli walikutana pamoja hapo Shilo, wakasimamisha hema ya kukutania huko; nayo nchi ilikuwa imeshindwa mbele zao. Yalikuwa yamebaki kati yao makabila saba ya wana wa Israeli ambayo yalikuwa hayajagawiwa urithi wao. Yoshua akawauliza wana wa Israeli, akasema, Je! Hata lini mtakuwa walegevu katika kuingia kwenu na kuimiliki hiyo nchi, ambayo yeye BWANA, Mungu wa baba zenu, amewapa?
Yoshua 18:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha mkutano mzima wa wana wa Israeli walikutana pamoja hapo Shilo, wakasimamisha hema ya kukutania kuko; nayo nchi ilikuwa imeshindwa mbele zao. Zilisalia katika wana wa Israeli kabila saba ambazo hazijagawanyiwa bado urithi wao. Yoshua akawauliza wana wa Israeli, akasema, Je! Hata lini mtakuwa walegevu katika kuingia kwenu na kuimiliki hiyo nchi, ambayo yeye BWANA, Mungu wa baba zenu, amewapa?
Yoshua 18:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kusanyiko lote la Waisraeli wakakusanyika huko Shilo na kusimamisha Hema la Kukutania. Nchi ikawa chini ya utawala wao, lakini palikuwa bado makabila saba ya Israeli ambayo yalikuwa hayajapokea urithi wao. Hivyo Yoshua akawaambia Waisraeli, “Je, mtasubiri hata lini ili kuingia kumiliki nchi ambayo BWANA, Mungu wa baba zenu, amewapa?