Yoshua 1:10-11
Yoshua 1:10-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Yoshua akawaamuru viongozi wa watu, “Piteni katika kambi na kuwaamrisha watu watayarishe chakula, kwa kuwa baada ya siku tatu mtavuka mto Yordani, kwenda kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawapeni iwe mali yenu.”
Yoshua 1:10-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo Yoshua akawaamuru viongozi wa watu, akisema, Piteni katika kambi, mkawaamuru hao watu, mkisema, Tayarisheni vyakula; kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, mpate kuimiliki.
Yoshua 1:10-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo Yoshua akawaamuru maakida wa watu, akisema, Piteni katikati ya matuo, mkawaamuru hao watu, mkisema, Fanyeni tayari vyakula; kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, mpate kuimiliki.
Yoshua 1:10-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo Yoshua akawaagiza maafisa wa watu akisema, “Pitieni katika kambi yote mkawaambie watu, ‘Tayarisheni vyakula vyenu. Siku tatu kuanzia sasa mtavuka Yordani ili kuingia na kuimiliki nchi ambayo BWANA Mungu wenu anawapa iwe yenu.’ ”