Yoshua 1:1-2
Yoshua 1:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya kifo cha Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi-Mungu alimwambia Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Mose: “Mtumishi wangu Mose amefariki, sasa vukeni mto Yordani, wewe pamoja na Waisraeli wote hadi kwenye nchi ile ambayo ninawapa.
Yoshua 1:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa BWANA, BWANA akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema, Musa mtumishi wangu amefariki; sasa ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hadi nchi niwapayo wana wa Israeli.
Yoshua 1:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa BWANA, BWANA akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema, Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli.
Yoshua 1:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baada ya kifo cha Musa mtumishi wa BWANA, BWANA akamwambia Yoshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Musa: “Mtumishi wangu Musa amekufa. Sasa basi, wewe na watu wote hawa jiandaeni kuvuka Mto Yordani kuingia nchi nitakayowapa Waisraeli karibuni.