Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yona 2:7-10 - Compare All Versions

Yona 2:7-10 BHN (Biblia Habari Njema)

Roho yangu ilipoanza kunitoka, nilikukumbuka, ee Mwenyezi-Mungu, sala yangu ikakufikia, katika hekalu lako takatifu. Watu wanaoabudu sanamu za miungu batili, huutupilia mbali uaminifu wao kwako. Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani, nitakutolea sadaka, na kutimiza nadhiri zangu. Mwenyezi-Mungu, ndiye aokoaye.” Basi, Mwenyezi-Mungu akamwamuru yule samaki, naye akamtapika Yona kwenye nchi kavu.

Shirikisha
Yona 2 BHN

Yona 2:7-10 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nilimkumbuka BWANA; Maombi yangu yakakufikia, Katika hekalu lako takatifu. Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe. Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa BWANA. BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona katika pwani.

Shirikisha
Yona 2 SRUV

Yona 2:7-10 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka BWANA; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu. Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe; Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa BWANA. BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.

Shirikisha
Yona 2 SUV

Yona 2:7-10 NEN (Neno)

“Uhai wangu ulipokuwa unatoka, nilikukumbuka wewe, BWANA, nayo maombi yangu yalikufikia wewe, katika Hekalu lako takatifu. “Wale watu wanaoshikilia sanamu batili hupoteza neema yao. Lakini mimi nitakutolea dhabihu, kwa sauti za shukrani na shangwe. Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza. Wokovu watoka kwa BWANA.” Basi BWANA akamwamuru yule samaki, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.

Shirikisha
Yona 2 NEN