Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yona 2:1-2 - Compare All Versions

Yona 2:1-2 BHN (Biblia Habari Njema)

Basi, Yona, akiwa tumboni mwa samaki huyo, akawa akimwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, akisema: “Kwa sababu ya taabu yangu, nilikuomba, ee Mwenyezi-Mungu, nawe ukanisikiliza; toka chini kuzimu, nilikulilia, nawe ukasikiliza kilio changu.

Shirikisha
Yona 2 BHN

Yona 2:1-2 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Ndipo Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, akiwa katika tumbo la yule samaki, Akasema, Nilimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu niliomba, Nawe ukasikia sauti yangu.

Shirikisha
Yona 2 SRUV

Yona 2:1-2 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Ndipo Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki, Akasema, Nalimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu.

Shirikisha
Yona 2 SUV

Yona 2:1-2 NEN (Neno)

Akiwa ndani ya tumbo la samaki, Yona alimwomba BWANA Mungu wake. Akasema: “Katika shida yangu nalimwita BWANA, naye akanijibu. Kutoka kina cha kaburi niliomba msaada, nawe ukasikiliza kilio changu.

Shirikisha
Yona 2 NEN