Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yona 1:1-3 - Compare All Versions

Yona 1:1-3 BHN (Biblia Habari Njema)

Siku moja, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yona, mwana wa Amitai: “Ondoka uende Ninewi, ule mji mkuu, ukaukemee, maana nimeona uovu wake ni mkubwa mno.” Basi, Yona akaanza safari, lakini akashika njia ya kwenda Tarshishi ili kumkwepa Mwenyezi-Mungu. Akaenda hadi mjini Yopa ambapo alikuta meli moja iko tayari kwenda Tarshishi. Alilipa nauli, akapanda meli, akasafiri na mabaharia hao kwenda Tarshishi ili kumkwepa Mwenyezi-Mungu.

Shirikisha
Yona 1 BHN

Yona 1:1-3 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Basi neno la BWANA lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu. Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa BWANA; akateremka hadi Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akalipa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa BWANA.

Shirikisha
Yona 1 SRUV

Yona 1:1-3 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Basi neno la BWANA lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu. Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa BWANA; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa BWANA.

Shirikisha
Yona 1 SUV

Yona 1:1-3 NEN (Neno)

Neno la BWANA lilimjia Yona mwana wa Amitai: “Nenda mji mkubwa wa Ninawi ukahubiri dhidi yake, kwa sababu uovu wake umefika kwangu.” Lakini Yona alimkimbia BWANA na kuelekea Tarshishi. Alishuka hadi Yafa, ambapo alikuta meli iliyokuwa imepangwa kuelekea bandari ile. Baada ya kulipa nauli, akapanda kwenye meli na kuelekea Tarshishi ili kumkimbia BWANA.

Shirikisha
Yona 1 NEN