Yoeli 3:9-11
Yoeli 3:9-11 Biblia Habari Njema (BHN)
“Watangazieni watu wa mataifa jambo hili: Jitayarisheni kwa vita, waiteni mashujaa wenu; askari wote na wakusanyike, waende mbele. Majembe yenu yafueni yawe mapanga, miundu yenu ya kupogolea iwe mikuki. Hata aliye dhaifu na aseme: ‘Mimi pia ni shujaa’. Njoni haraka, enyi mataifa yote jirani, kusanyikeni huko bondeni.” Ee Mwenyezi-Mungu! Teremsha askari wako dhidi yao!
Yoeli 3:9-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tangazeni haya kati ya mataifa; jitayarisheni kwa vita; waamsheni mashujaa; watu wa vita na wakaribie; na wapande juu. Yafueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari. Fanyeni haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande zote, jikusanyeni pamoja; na huko wateremshe mashujaa wako wote, Ee BWANA.
Yoeli 3:9-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tangazeni haya kati ya mataifa; takaseni vita; waamsheni mashujaa; watu wa vita na wakaribie; na wapande juu. Yafueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari. Fanyeni haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande zote, jikusanyeni pamoja; na huko watelemshe mashujaa wako wote, Ee BWANA.
Yoeli 3:9-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Tangazeni hili miongoni mwa mataifa: Jiandaeni kwa vita! Amsha mashujaa! Wapiganaji wote wasogee karibu na kushambulia. Majembe yenu yafueni yawe panga, na miundu yenu ya kukatia iwe mikuki. Aliye dhaifu na aseme, “Mimi nina nguvu!” Njooni haraka, ninyi mataifa yote kutoka pande zote, kusanyikeni huko.