Yoeli 2:24-25
Yoeli 2:24-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Mahali pa kupuria patajaa nafaka, mashinikizo yatafurika divai na mafuta. Nitawarudishia miaka ile iliyoliwa na nzige, kila kitu kilicholiwa na tunutu, parare na matumatu, hilo jeshi kubwa nililowaletea!
Shirikisha
Soma Yoeli 2Yoeli 2:24-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta. Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.
Shirikisha
Soma Yoeli 2