Yoeli 2:1-2
Yoeli 2:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Pigeni tarumbeta huko Siyoni; pigeni baragumu juu ya mlima mtakatifu! Tetemekeni enyi wakazi wa Yuda, maana siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja, naam, siku hiyo iko karibu! Hiyo ni siku ya giza na huzuni; siku ya mawingu na giza nene. Jeshi kubwa la nzige linakaribia kama giza linalotanda milimani. Namna hiyo haijapata kuweko kamwe wala haitaonekana tena katika vizazi vyote vijavyo.
Yoeli 2:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia; siku ya giza na huzuni, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.
Yoeli 2:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia; siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.
Yoeli 2:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Pigeni tarumbeta katika Sayuni; pigeni mbiu katika mlima wangu mtakatifu. Wote wanaoishi katika nchi na watetemeke, kwa kuwa siku ya BWANA inakuja. Iko karibu, siku ya giza na huzuni, siku ya mawingu na utusitusi. Kama mapambazuko yanavyosambaa toka upande huu wa milima hata upande mwingine, jeshi kubwa na lenye nguvu linakuja. Jambo kama hili halijakuwepo tangu zamani, wala halitakuwepo tena kamwe kwa vizazi vijavyo.