Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 9:1-20

Yobu 9:1-20 Biblia Habari Njema (BHN)

Kisha Yobu akajibu: “Kweli najua hivyo ndivyo ilivyo. Lakini mtu awezaje kuwa mwema mbele ya Mungu? Kama mtu angethubutu kushindana naye, hataweza kufika mbali; hata kujibu swali moja kati ya elfu. Yeye ni mwenye hekima mno na nguvu nyingi, nani aliyepingana naye, akashinda? Yeye huiondoa milima bila yenyewe kutambua, huibomolea mbali kwa hasira yake. Yeye huitikisa dunia kutoka mahali pake, na nguzo zake zikatetemeka. Huliamuru jua lisichomoze huziziba nyota zisiangaze. Yeye peke yake alizitandaza mbingu, na kuyakanyaga mawimbi ya bahari. Ndiye aliyezifanya nyota angani: Dubu, Orioni, Kilimia, na nyota za kusini. Ndiye atendaye makuu yasiyoeleweka, mambo ya ajabu yasiyo na idadi. Loo! Hupita karibu nami nisimwone, kisha huenda zake bila ya mimi kumtambua. Tazama! Yeye huchukua anachotaka; nani awezaye kumzuia? Nani awezaye kumwuliza: ‘Unafanya nini?’ “Mungu hatazuia hasira yake; chini yake wainama kwa hofu Rahabu na wasaidizi wake. Nitawezaje basi kumjibu Mungu? Nitachagua wapi maneno ya kumwambia? Ingawa sina hatia, siwezi kumjibu. Lazima kumwomba anihurumie huyo mshtaki wangu. Hata kama ningemwita naye akajibu, nisingeweza kuamini kuwa ananisikiliza. Yeye huniponda kwa dhoruba; huongeza majeraha yangu bila sababu. Haniachi hata nipumue; maisha yangu huyajaza uchungu. Kama ni kushindana, yeye ana nguvu mno! Na kama ni kutafuta juu ya haki, nani atakayemleta mahakamani? Ingawa sina hatia, maneno yangu yenyewe yangenihukumu; ingawa sina lawama, angenithibitisha kuwa mpotovu.

Shirikisha
Soma Yobu 9

Yobu 9:1-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, Kweli najua kuwa ndivyo hivyo; Lakini mtu huwaje mwenye haki mbele za Mungu? Kama akipenda kushindana naye, Hawezi kumjibu neno moja katika elfu. Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa? Aiondoaye milima, nayo haina habari, Akiipindua katika hasira zake. Aitikisaye dunia itoke mahali pake, Na nguzo zake hutetemeka. Aliamuruye jua, nalo halichomozi; Nazo nyota huzipiga mhuri. Ambaye peke yake ni mwenye kuzitandika mbingu, Na kuyakanyaga mawimbi ya bahari. Yeye afanyaye hizo nyota za Dubu, na Orioni, na hicho Kilimia, Na makundi ya nyota ya kusini. Atendaye mambo makuu yasiyochunguzika; Naam, mambo ya ajabu yasiyohesabika. Tazama, yuaenda karibu nami, nisimwone; Tena yuapita kwenda mbele, nisimtambue. Tazama, yuanyakua, ni nani awezaye kumzuia? Ni nani awezaye kumwuliza, Wafanya nini? Mungu haondoi hasira zake; Hao wamsaidiao Rahabu huinama chini yake. Je! Mimi nitamjibuje, Na kuyachagua maneno yangu kuhojiana naye? Ambaye, nijapokuwa mimi ni mwenye haki, siwezi kumjibu; Ni lazima nimwombe mshitaki wangu anihurumie. Kama ningemwita, naye akaniitikia; Hata hivyo singeamini kuwa amesikiza sauti yangu. Yeye anipondaye kwa dhoruba, Na kuyaongeza majeraha yangu pasipokuwa na sababu. Haniachi nipate kuvuta pumzi, Lakini hunijaza uchungu. Kama tukitaja nguvu za mashujaa, tazama yupo hapo! Kama tukitaja hukumu, ni nani atakayemwita mahakamani? Ingawa mimi ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; Ingawa mimi ni mkamilifu, kitanishuhudia kuwa mimi ni mpotovu.

Shirikisha
Soma Yobu 9

Yobu 9:1-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, Kweli najua kuwa ndivyo hivyo; Lakini mtu huwaje mwenye haki mbele za Mungu? Kama akipenda kushindana naye, Hawezi kumjibu neno moja katika elfu. Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa? Aiondoaye milima, nayo haina habari, Akiipindua katika hasira zake. Aitikisaye dunia itoke mahali pake, Na nguzo zake hutetema. Aliamuruye jua, nalo halichomozi; Nazo nyota huzipiga muhuri. Ambaye peke yake ni mwenye kuzitandika mbingu, Na kuyakanyaga mawimbi ya bahari. Yeye afanyaye hizo nyota za Dubu, na Orioni, na hicho Kilimia, Na makundi ya nyota ya kusini. Atendaye mambo makuu yasiyotafutikana; Naam, mambo ya ajabu yasiyohesabika. Tazama, yuaenenda karibu nami, nisimwone; Tena yuapita kwenda mbele, nisimtambue. Tazama, yuakamata, ni nani awezaye kumzuia? Ni nani awezaye kumwuliza, Wafanya nini? Mungu haondoi hasira zake; Hao wamsaidiao Rahabu huinama chini yake. Je! Mimi nitamjibuje, Na kuyachagua maneno yangu kuhojiana naye? Ambaye, nijapokuwa mimi ni mwenye haki, nisingemjibu; Ningemsihi-sihi mtesi wangu. Kama ningemwita, naye akaniitikia; Hata hivyo singeamini kuwa amesikiza sauti yangu. Yeye anipondaye kwa dhoruba, Na kuziongeza jeraha zangu pasipokuwa na sababu. Haniachi nipate kuvuta pumzi, Lakini hunijaza uchungu. Kama tukitaja nguvu za mashujaa, tazama yupo hapo! Kama tukitaja hukumu, ni nani atakayeniwekea muhula? Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; Ingawa ni mkamilifu, kitanishuhudia kuwa ni mpotovu.

Shirikisha
Soma Yobu 9

Yobu 9:1-20 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Kisha Ayubu akajibu: “Naam, najua hili ni kweli. Lakini mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? Ingawa mtu angetaka kushindana naye, hangeweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja. Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno. Ni nani aliyempinga naye akawa salama? Aiondoa milima bila yenyewe kujua na kuipindua kwa hasira yake. Aitikisa dunia kutoka mahali pake na kuzifanya nguzo zake zitetemeke. Husema na jua, nalo likaacha kuangaza; naye huizima mianga ya nyota. Yeye peke yake huzitandaza mbingu na kuyakanyaga mawimbi ya bahari. Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu, na Orioni, Kilimia, na makundi ya nyota za kusini. Hutenda maajabu yasiyopimika, miujiza isiyoweza kuhesabiwa. Anapopita karibu nami, siwezi kumwona; apitapo mbele yangu, simtambui. Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia? Ni nani awezaye kumwambia, ‘Unafanya nini?’ Mungu hataizuia hasira yake; hata jeshi kubwa la Rahabu lenye nguvu linajikunyata miguuni pake. “Ni vipi basi mimi nitaweza kubishana naye? Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye? Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu; ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie. Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali, siamini kama angenisikiliza. Yeye angeniangamiza kwa dhoruba na kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu. Asingeniacha nipumue bali angenifunika kabisa na huzuni kuu. Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu! Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani? Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu; kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia.

Shirikisha
Soma Yobu 9