Yobu 8:2-13
Yobu 8:2-13 Biblia Habari Njema (BHN)
“Utasema mambo haya mpaka lini? Mpaka lini maneno yako yatakuwa matupu kama upepo? Kwani, wadhani Mungu hupotosha haki? Au, je, Mungu Mwenye Nguvu hupotosha ukweli? Kama watoto wako wamemkosea Mungu, yeye amewalipiza matokeo ya uhalifu wao. Kama utamtafuta Mungu ukamsihi huyo Mungu mwenye nguvu, kama wewe u safi moyoni na mnyofu, kweli Mungu atakuja kukusaidia, na kukujalia makao unayostahili. Na ingawa ulianza kuishi kwa unyonge maisha yako ya baadaye yatakuwa ya fahari zaidi. Jifunze tafadhali kwa wale waliotutangulia, zingatia mambo waliyogundua hao wazee. Sisi ni watu wa juzijuzi tu, hatujui kitu; siku zetu duniani ni kivuli kipitacho. Lakini wao watakufunza na kukuambia, mambo waliyopata kuyatoa katika maarifa yao: Mafunjo huota tu penye majimaji, matete hustawi mahali palipo na maji. Hata kama yamechanua na bila kukatwa, yakikosa maji hunyauka kabla ya mimea mingine. Ndivyo walivyo wote wanaomsahau Mungu. Tumaini la wasiomwamini Mungu litapotea.
Yobu 8:2-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wewe utanena maneno haya hadi lini? Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hadi lini? Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki? Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao; Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; Ikiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa. Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana. Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta; (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;) Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza, Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao? Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope Na makangaga kumea pasipo maji? Yakiwa yangali mabichi bado, wala hayakukatwa, Hunyauka mbele ya majani mengine. Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; Na matumaini yake huyo mbaya huangamia
Yobu 8:2-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wewe utanena maneno haya hata lini? Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hata lini? Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki? Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao; Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa. Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana. Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta; (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;) Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza, Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao? Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope Na makangaga kumea pasipo maji? Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa, Hunyauka mbele ya majani mengine. Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; Na matumaini yake huyo mbaya huangamia
Yobu 8:2-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Hata lini wewe utasema mambo kama haya? Maneno yako ni kama upepo mkuu. Je, Mungu hupotosha hukumu? Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki? Watoto wako walipomtenda dhambi, aliwapa adhabu ya dhambi yao. Lakini ukimtafuta Mungu, nawe ukamsihi Mwenyezi, ikiwa wewe ni safi na mnyofu, hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako, na kukurudisha katika mahali pako pa haki. Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo, lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio. “Ukaulize vizazi vilivyotangulia na uone baba zao walijifunza nini, kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote, nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu. Je, hawatakufundisha na kukueleza? Je, hawataleta maneno ya ufahamu wao? Je, mafunjo yaweza kumea mahali pasipo na matope? Matete yaweza kustawi bila maji? Wakati bado yanaendelea kukua kabla ya kukatwa, hunyauka haraka kuliko majani mengine. Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu; vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.