Yobu 7:1-7
Yobu 7:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
“Binadamu anayo magumu duniani, na siku zake ni kama siku za kibarua! Yeye ni kama mtumwa atamaniye kivuli, kama mwajiriwa angojaye kwa hamu mshahara wake. Basi nimepangiwa miezi na miezi ya ubatili, yangu ni majonzi usiku hata usiku. Nilalapo nasema, ‘Nitaamka lini?’ Kwani saa za usiku huwa ndefu sana; nagaagaa kitandani mpaka kuche! Mwili wangu umejaa mabuu na uchafu; ngozi yangu imekauka na kutokwa na usaha wa jipu. Siku zangu zapita kasi kuliko gurudumu la mshonaji, nazo zafikia mwisho wake bila matumaini. “Kumbuka, maisha yangu ni pumzi tu; jicho langu halitaona jema lolote tena.
Yobu 7:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Je! Mtu hana huduma ngumu juu ya nchi? Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa? Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli, Kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake; Hivyo basi nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu, Nami nimeandikiwa mateso usiku hata usiku. Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke. Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena. Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini. Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; Jicho langu halitaona mema tena.
Yobu 7:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi? Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa? Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli, Kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake; Ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu, Nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha. Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke. Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena. Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini. Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; Jicho langu halitaona mema tena.
Yobu 7:1-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Je, mwanadamu hana kazi ngumu duniani? Siku zake si kama zile za mtu aliyeajiriwa? Kama mtumwa anavyovionea shauku vivuli vya jioni, au mtu aliyeajiriwa anavyoungojea mshahara wake, ndivyo nilivyogawiwa miezi ya ubatili, nami nimeandikiwa huzuni usiku hata usiku. Nilalapo ninawaza, ‘Itachukua muda gani kabla sijaamka?’ Usiku huwa mrefu, nami najigeuzageuza hadi mapambazuko. Mwili wangu umevikwa mabuu na uchafu, ngozi yangu imetumbuka na kutunga usaha. “Siku zangu zinapita upesi kuliko mtande wa kufuma, nazo zinafikia mwisho wake bila matumaini. Kumbuka, Ee Mungu, maisha yangu ni kama pumzi; macho yangu kamwe hayataona tena raha.