Yobu 5:8-18
Yobu 5:8-18 Biblia Habari Njema (BHN)
“Kama ningekuwa wewe ningemgeukia Mungu, ningemwekea yeye Mungu kisa changu, yeye atendaye makuu yasiyochunguzika, atendaye maajabu yasiyohesabika. Huinyeshea nchi mvua, hupeleka maji mashambani. Huwainua juu walio wanyonge, wenye kuomboleza huwapa usalama. Huvunja mipango ya wenye hila, matendo yao yasipate mafanikio. Huwanasa wenye hekima kwa werevu wao, mipango ya wajanja huikomesha mara moja. Hao huona giza wakati wa mchana, adhuhuri hupapasapapasa kama vile usiku. Lakini Mungu huwaokoa yatima wasiuawe, huwanyakua fukara mikononi mwa wenye nguvu. Hivyo maskini wanalo tumaini, nao udhalimu hukomeshwa. “Heri mtu yule ambaye Mungu anamrudi! Hivyo usidharau Mungu Mwenye Nguvu anapokuadhibu. Kwani yeye huumiza na pia huuguza; hujeruhi, na kwa mkono wake huponya.
Yobu 5:8-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini mimi ningemtafuta Mungu, Ningemwekea Mungu kesi yangu; Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana; Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu; Yeye atoaye mvua inyeshe juu ya nchi, Na kuyapeleka maji mashambani; Awainuaye juu hao walio chini; Na hao waombolezao hukuzwa wawe salama. Yeye huitangua mipango ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao. Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka. Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vile vile kama usiku. Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari. Basi hivi huyo maskini ana matumaini, Na uovu hufumba kinywa chake. Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye; Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi. Kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza; Yeye hutia jeraha, na mikono yake huponya.
Yobu 5:8-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini mimi ningemtafuta Mungu, Ningemwekea Mungu daawa yangu; Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana; Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu; Yeye atoaye mvua inyeshe juu ya nchi, Na kuyapeleka maji mashambani; Awainuaye juu hao walio chini; Na hao waombolezao hukuzwa wawe salama. Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao. Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka. Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vilevile kama usiku. Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari. Basi hivi huyo maskini ana matumaini, Na uovu hufumba kinywa chake. Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye; Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi. Kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza; Yeye hutia jeraha, na mikono yake huponya.
Yobu 5:8-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu, ningeweka shauri langu mbele zake. Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, miujiza isiyoweza kuhesabika. Yeye huipa nchi mvua, huyapeleka maji kunyesha mashamba. Huwainua juu wanyonge, nao wale wanaoomboleza huinuliwa wakawa salama. Huipinga mipango ya wenye hila, ili mikono yao isifikie ufanisi. Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao, nayo mipango ya wadanganyifu huifagilia mbali. Giza huwapata wakati wa mchana; wakati wa adhuhuri hupapasa kama vile usiku. Humwokoa mhitaji kutokana na upanga ulioko kinywani mwao; huwaokoa kutokana na makucha ya wenye nguvu. Kwa hiyo maskini analo tarajio, nao udhalimu hufumba kinywa chake. “Heri mtu yule ambaye Mungu humkanya; kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi. Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga; huumiza, lakini mikono yake pia huponya.