Yobu 42:3-6
Yobu 42:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Ulisema kuwa nilithubutu kutatiza mpango wako kijinga. Kweli nilitamka kitu ambacho sikuelewa mambo ya ajabu mno kwangu ambayo sikuwa ninayajua. Uliniambia nisikilize nawe utaniambia; kwamba utaniuliza nami nikujibu. Kweli nilikuwa nimesikia habari zako kwa masikio tu, lakini sasa nakuona kwa macho yangu mwenyewe. Kwa hiyo natubu pamoja na kujipaka mavumbi na majivu, najiona mimi mwenyewe kuwa si kitu kabisa.”
Yobu 42:3-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ni nani huyu afichaye ushauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua. Sikiliza, nakusihi, nami nitanena; Nitakuuliza neno, nawe niambie. Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona. Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu Katika mavumbi na majivu.
Yobu 42:3-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua. Sikiliza, nakusihi, nami nitanena; Nitakuuliza neno, nawe niambie. Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona. Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu Katika mavumbi na majivu.
Yobu 42:3-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’ Hakika nilisema mambo nisiyoyaelewa, mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua. “Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena; nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’ Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako, lakini sasa macho yangu yamekuona. Kwa hiyo najidharau mwenyewe, na kutubu katika mavumbi na majivu.”