Yobu 42:1-3
Yobu 42:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Yobu akamjibu Mwenyezi-Mungu: “Najua kwamba waweza kila kitu, lolote unalokusudia haliwezi kuzuiliwa. Ulisema kuwa nilithubutu kutatiza mpango wako kijinga. Kweli nilitamka kitu ambacho sikuelewa mambo ya ajabu mno kwangu ambayo sikuwa ninayajua.
Yobu 42:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo Ayubu akamjibu BWANA, na kusema. Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. Ni nani huyu afichaye ushauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua.
Yobu 42:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo Ayubu akamjibu BWANA, na kusema. Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua.
Yobu 42:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo Ayubu akamjibu BWANA: “Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote, wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika. Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’ Hakika nilisema mambo nisiyoyaelewa, mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua.