Yobu 41:1-6
Yobu 41:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
“Yeyote anayeliona hilo dude, hufa moyo na kuzirai. Hakuna mtu yeyote mkali athubutuye kulishtua. Nani, basi awezaye kusimama mbele yangu? Nani aliyenipa kitu, ili nitakiwe kumrudishia? Chochote kilicho chini ya mbingu ni changu. “Sitaacha kukueleza juu ya viungo vya hilo dude au juu ya nguvu zake na umbo lake zuri. Nani awezaye kumbambua vazi lake la nje? Nani awezaye kutoboa deraya lililovaa? Nani awezaye kufungua kinywa chake? Meno yake pande zote ni kitisho!
Yobu 41:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana? Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba? Je! Waweza kutia kamba puani mwake? Au kutoboa taya yake kwa kulabu? Je! Atakusihi sana? Au, atakuambia maneno ya upole? Je! Atafanya agano pamoja nawe, Umtwae kuwa mtumishi wako milele? Je! Utamchezea kama ndege? Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako? Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara? Watamgawanya kati ya wafanyao biashara?
Yobu 41:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana? Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba? Je! Waweza kutia kamba puani mwake? Au kutoboa taya yake kwa kulabu? Je! Atakusihi sana? Au, atakuambia maneno ya upole? Je! Atafanya agano pamoja nawe, Umtwae kuwa mtumishi wako milele? Je! Utamchezea kama ndege? Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako? Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara? Watamgawanya kati ya wafanyao biashara?
Yobu 41:1-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Je, unaweza kumvua Lewiathani kwa ndoana ya samaki, au kufunga ulimi wake kwa kamba? Unaweza kupitisha kamba puani mwake, au kutoboa taya lake kwa kulabu? Je, ataendelea kukuomba umhurumie? Atasema nawe maneno ya upole? Je, atafanya agano nawe ili umtwae awe mtumishi wako maisha yake yote? Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege, au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako? Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake? Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara?