Yobu 40:1-5
Yobu 40:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu akaendelea kumwambia Yobu: “Je, wewe mwenye kuchunguza makosa utashindana na Mungu Mwenye Nguvu? Wewe unayebishana nami Mungu, basi jibu mambo hayo!” Kisha Yobu akamjibu Mwenyezi-Mungu: “Mimi sifai kitu nitakujibu nini? Naufunga mdomo wangu. Nilithubutu kusema na sitasema tena. Nilisisitiza lakini sitaendelea kusema zaidi.”

Yobu 40:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akafululiza kumjibu Ayubu, na kusema, Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye. Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema, Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini? Naweka mkono wangu kinywani pangu. Nimenena mara moja, nami sitajibu; Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.
Yobu 40:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akafuliza kumjibu Ayubu, na kusema, Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye. Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema, Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini? Naweka mkono wangu kinywani pangu. Nimenena mara moja, nami sitajibu; Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.
Yobu 40:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA akamwambia Ayubu: “Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha? Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.” Ndipo Ayubu akamjibu BWANA: “Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe? Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu. Nimesema mara moja, lakini sina jibu; naam, nimesema mara mbili, lakini sitasema tena.”