Yobu 4:1-8
Yobu 4:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Elifazi yule Mtemani akamjibu Yobu: “Je, mtu akijaribu kukuambia neno utakasirika? Lakini nani awezaye kujizuia kusema? Sikiliza! Wewe umewafundisha wengi, na kuiimarisha mikono ya wanyonge. Maneno yako yamewainua waliokufa moyo, umewaimarisha waliokosa nguvu. Lakini sasa yamekupata, nawe ukakosa subira, yamekugusa, nawe ukafadhaika. Je, kumcha Mungu si ndilo tegemeo lako? Na unyofu wako si ndilo tumaini lako? Fikiri sasa: Nani asiye na hatia ambaye amepata kuangamia? Au, je, waadilifu wamepata kutupwa? Nijuavyo mimi, wapandao uovu na ubaya huvuna hayohayo
Yobu 4:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo huyo Elifazi, Mtemani, akajibu na kusema, Mtu akijaribu kuzungumza nawe, je! Utaona ni vibaya? Lakini ni nani awezaye kujizuia asinene? Tazama, wewe umewafunza watu wengi, Nawe umeitia nguvu mikono iliyokuwa minyonge. Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka, Nawe umeyaimarisha magoti manyonge. Lakini sasa haya yamekufikia wewe, nawe wafa moyo; Yamekugusa, nawe wafadhaika. Je! Dini yako siyo tegemeo lako? Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako? Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au ni wapi hao waelekevu walikatiliwa mbali? Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo.
Yobu 4:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo huyo Elifazi, Mtemani, akajibu na kusema, Mtu akijaribu kuzungumza nawe, je! Utaona ni vibaya? Lakini ni nani awezaye kujizuia asinene? Tazama, wewe umewafunza watu wengi, Nawe umeitia nguvu mikono iliyokuwa minyonge. Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka, Nawe umeyaimarisha magoti manyonge. Lakini sasa haya yamekufikilia wewe, nawe wafa moyo; Yamekugusa, nawe wafadhaika. Je! Dini yako siyo mataraja yako, Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako? Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi? Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo.
Yobu 4:1-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo Elifazi Mtemani akajibu: “Kama mtu akithubutu kuzungumza nawe, kutakukasirisha? Lakini ni nani awezaye kujizuia asiseme? Fikiri jinsi umewafundisha watu wengi, jinsi umeitia nguvu mikono iliyokuwa dhaifu. Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa; umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu. Lakini sasa hii taabu imekujia wewe, nawe unashuka moyo; imekupiga wewe, nawe unafadhaika. Je, kumcha Mungu kwako hakupaswi kuwa ndiyo matumaini yako na njia zako kutokuwa na lawama ndilo taraja lako? “Fikiri sasa: Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia? Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa? Kwa jinsi mimi nimechunguza, wale walimao ubaya na wale hupanda uovu, huvuna hayo hayo.