Yobu 38:1-41
Yobu 38:1-41 Biblia Habari Njema (BHN)
Hapo Mwenyezi-Mungu alimjibu Yobu kutoka dhoruba: “Nani wewe unayevuruga mashauri yangu kwa maneno yasiyo na akili? Jikaze kama mwanamume, nami nitakuuliza nawe utanijibu. “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia? Niambie, kama una maarifa. Ni nani aliyeweka vipimo vyake, wajua bila shaka! Au nani aliyelaza kamba juu yake kuipima? Je, nguzo za dunia zimesimikwa juu ya nini, au nani aliyeliweka jiwe lake la msingi, nyota za asubuhi zilipokuwa zikiimba pamoja, na wana wa Mungu wakapaza sauti za shangwe? Ni nani aliyeyafunga mafuriko ya bahari wakati yalipozuka na kuvuma kutoka vilindini? Mimi ndiye niliyeifunika bahari kwa mawingu na kuiviringishia giza nene. Niliiwekea bahari mipaka, nikaizuia kwa makomeo na milango, nikaiambia: ‘Mwisho wako ni hapa, si zaidi! Mawimbi yako ya nguvu yatakomea hapa!’ “Yobu, tangu uzaliwe umewahi kuamuru kupambazuke? na kulifanya pambazuko lijue mahali pake, ili lipate kuikamata dunia kwa pembe zake na kuwatimulia mbali waovu waliomo? Dunia hugeuka na kupata rangi kama vazi; kama udongo wa mfinyanzi unavyogeuzwa na mhuri. Lakini waovu watanyimwa mwanga wao, mkono wanaonyosha kupiga watu utavunjwa. “Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari? au kutembea juu ya sakafu ya kilindi cha bahari? Je, umewahi kuoneshwa malango ya kifo, au kuyaona malango ya makazi ya giza nene? Je, wajua ukubwa wa dunia? Niambie kama unajua haya yote. “Je, makao ya mwanga yako wapi? Nyumbani kwa giza ni wapi, ili upate kulipeleka kwenye makao yake, na kuifahamu njia ya kwenda huko kwake. Wewe unapaswa kujua, wewe ambaye umekwisha ishi miaka mingi! “Je, umewahi kuingia katika bohari za theluji, au kuona bohari za mvua ya mawe ambavyo nimevihifadhi kwa ajili ya wakati wa fujo, kwa ajili ya siku ya mapigano na vita? Ipi njia ya kwenda mahali mwanga unapogawanywa, au huko kunakotoka upepo wa mashariki ukasambazwa duniani? “Nani aliyechora angani njia kwa ajili ya mvua? Nani aliyeionesha radi njia yake mawinguni, ikasababisha mvua kunyesha nchini kusikoishi mtu na jangwani ambako hakuna mtu, ili kuiburudisha nchi kavu na kame na kuifanya iote nyasi? “Je, mvua ina baba? Au nani ameyazaa matone ya umande? Je, barafu ilitoka tumboni kwa nani? Nani aliyeizaa theluji? Maji hugeuka kuwa magumu kama jiwe, na uso wa bahari ukaganda. “Angalia makundi ya nyota: Je, unaweza kuifunga minyororo Kilimia, au kuvilegeza vifungo vya Orioni? Je, waweza kuziongoza nyota katika majira yake, au kumwongoza Dubu pamoja na watoto wake? Je, wazijua kanuni zinazotawala mbingu; Je, waweza kuzipangia taratibu zao duniani? “Je, waweza kupaza sauti na kuyaamuru mawingu yakufunike kwa mtiririko wa mvua? Je, wewe ukiamuru umeme umulike, utakujia na kusema: ‘Nipo hapa?’ Ni nani aliyemjulisha kwarara kujaa kwa mto Nili au aliyemwambia jogoo kwamba mvua inakuja? Nani mwenye akili ya kuweza kuhesabu mawingu, au kuinamisha viriba vya maji huko mbinguni? ili vumbi duniani igandamane na udongo ushikamane na kuwa matope? “Je, waweza kumwindia simba mawindo yake au kuishibisha hamu ya wana simba; wanapojificha mapangoni mwao, au kulala mafichoni wakiotea? Ni nani awapaye kunguru chakula chao, makinda yao yanaponililia mimi Mungu, na kurukaruka huku na huko kwa njaa?
Yobu 38:1-41 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Ni nani huyu atiaye ushauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa? Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie. Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama una ufahamu. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake – hakika unajua! Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake? Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha? Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipotoka kwa nguvu kama kwamba imetoka tumboni mwa nchi. Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia, Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomeo na milango, Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yenye nguvu yatazuiliwa? Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake? Yapate kuishika miisho ya nchi, Waovu wakung'utwe wakawe mbali nayo? Hubadilika mfano wa udongo chini ya mhuri, Vitu vyote vinatokea kama mavazi. Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie, Na mkono ulioinuka huvunjika. Je! Umeziingia chemchemi za bahari, Au umetembea mahali pa siri pa vilindi? Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu? Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote. Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi? Upate kuipeleka hata mpaka wake, Upate kuyaelewa mapito ya kuiendea nyumba yake? Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo, Na hesabu ya siku zako ni kubwa! Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe, Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, Kwa siku ya mapigano na vita? Je! Nuru hutengwa kwa njia gani, Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi? Ni nani aliyepasua mfereji kwa maji ya gharika, Au njia kwa umeme wa radi; Kunyesha mvua juu ya nchi isiyo na watu; Juu ya jangwa asiyokaa mwanadamu; Kuishibisha nchi iliyo kame na ukiwa, Na kuyameza majani yaliyo mororo? Je! Mvua ina baba? Au ni nani aliyeyazaa matone ya umande? Barafu ilitoka katika tumbo la nani? Na sakitu ya mbinguni ni nani aliyeizaa? Maji hugandamana kama jiwe, Na uso wa vilindi huganda kwa baridi. Je! Waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia, Au kuvilegeza vifungo vya Orioni? Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake? Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake? Je! Unazijua amri zilizoamriwa mbingu? Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia? Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, ili wingi wa maji ukufunikize? Waweza kuutuma umeme, nao ukaenda, Ukakuambia, Sisi tupo hapa? Je! Ni nani aliyetia hekima moyoni? Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni? Ni nani awezaye kuyahesabu mawingu kwa hekima? Au ni nani awezaye kuzimimina chupa za mbinguni? Wakati mavumbi yagandamanapo, Na madongoa kushikamana pamoja? Je! Utamwindia simba mke mawindo? Au utashibisha njaa ya simba wachanga, Waoteapo mapangoni mwao, Wakaapo mafichoni wapate kuvizia? Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutangatanga kwa kutindikiwa na chakula?
Yobu 38:1-41 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa? Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie. Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake? Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha? Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni. Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia, Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomeo na milango, Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yanyetayo yatazuiliwa? Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake? Yapate kuishika miisho ya nchi, Waovu wakung’utwe wakawe mbali nayo? Hubadilika mfano wa udongo chini ya muhuri, Vitu vyote vinatokea kama mavazi. Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie, Na mkono ulioinuka huvunjika. Je! Umeziingia chemchemi za bahari, Au umetembea mahali pa siri pa vilindi? Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu? Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote. Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi? Upate kuipeleka hata mpaka wake, Upate kuelewa na mapito ya kuiendea nyumba yake? Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo, Na hesabu ya siku zako ni kubwa! Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe, Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, Kwa siku ya mapigano na vita? Je! Nuru hutengwa kwa njia gani, Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi? Ni nani aliyepasua mfereji kwa maji ya gharika, Au njia kwa umeme wa radi; Kunyesha mvua juu ya nchi isiyo na watu; Juu ya jangwa asiyokaa mwanadamu; Kuishibisha nchi iliyo kame na ukiwa, Na kuyameza majani yaliyo mororo? Je! Mvua ina baba? Au ni nani aliyeyazaa matone ya umande? Barafu ilitoka katika tumbo la nani? Na sakitu ya mbinguni ni nani aliyeizaa? Maji hugandamana kama jiwe, Na uso wa vilindi huganda kwa baridi. Je! Waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia, Au kuvilegeza vifungo vya Orioni? Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake? Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake? Je! Unazijua amri zilizoamuriwa mbingu? Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia? Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, ili wingi wa maji ukufunikize? Waweza kuutuma umeme, nao ukaenda, Ukakuambia, Sisi tupo hapa? Je! Ni nani aliyetia hekima moyoni? Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni? Ni nani awezaye kuyahesabu mawingu kwa hekima? Au ni nani awezaye kuzimimina chupa za mbinguni? Wakati mavumbi yagandamanapo, Na madongoa kushikamana pamoja? Je! Utamwindia simba mke mawindo? Au utashibisha njaa ya simba wachanga, Waoteapo mapangoni mwao, Wakaapo mafichoni wapate kuvizia? Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutanga-tanga kwa kutindikiwa na chakula?
Yobu 38:1-41 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha BWANA akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema: “Nani huyu atiaye mashauri yangu giza kwa maneno yasiyo na maarifa? Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza swali, nawe unijibu. “Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia? Niambie, kama unafahamu. Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake? Hakika wewe unajua! Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake? Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini, au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni, wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na malaika wote walipokuwa wakishangilia kwa furaha? “Ni nani aliyeifungia bahari milango ilipopasuka kutoka tumbo, nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake, na kuyafungia katika giza nene, nilipoamuru mipaka yake, na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake, niliposema, ‘Unaweza kufika hapa, wala si zaidi; hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’? “Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke, au kuyaonesha mapambazuko mahali pake, yapate kushika miisho ya dunia, na kuwakungʼuta waovu waliomo? Dunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya muhuri; sura yake hukaa kama ile ya vazi. Waovu huzuiliwa nuru yao, nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa. “Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari? Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi? Umewahi kuoneshwa malango ya mauti? Umewahi kuiona milango ya uvuli wa mauti? Je, wewe unafahamu ukubwa wa dunia? Niambie kama unajua haya yote. “Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi? Nako maskani mwa giza ni wapi? Je, unaweza kuvirudisha kwenye makao yake? Unajua njia za kufika maskani mwake? Hakika unajua, kwa kuwa ulikuwa umeshazaliwa! Kwani umeishi miaka mingi! “Je, umeshawahi kuingia katika maghala ya theluji, au kuona maghala ya mvua ya mawe, ambazo nimeziweka akiba kwa ajili ya wakati wa taabu, na kwa ajili ya wakati wa vita na mapigano? Njia iendayo mahali miali ya radi inapotawanywa ni ipi, au njia iendayo mahali upepo wa mashariki unaposambazwa juu ya dunia? Ni nani aliyepasua mifereji kwa ajili ya maji mengi ya mvua yaendayo kasi na njia ya miali ya radi, ili kusababisha mvua kunyeshea mahali pasipokaliwa na mtu, jangwa lisilo na yeyote ndani yake, ili kuitosheleza nchi ya ukiwa na jangwa, na majani yaanze kumea ndani yake? Je, mvua ina baba? Ni nani baba azaaye matone ya umande? Barafu inatoka tumbo la nani? Ni nani azaaye ukungu kutoka mbinguni, wakati maji yanakuwa magumu kama jiwe, wakati uso wa vilindi vya maji unaganda? “Je, unaweza kuufunga mnyororo wa Kilimia? Unaweza kulegeza kamba za Orioni? Unaweza kuyaongoza makundi ya nyota kwa majira yake, au kuongoza Dubu na watoto wake? Je, unajua sheria zinazotawala mbingu? Unaweza kuweka utawala wa Mungu duniani? “Unaweza kuipaza sauti yako hadi mawinguni, na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji? Je, wewe hutuma miali ya radi kwenye njia zake? Je, hutoa taarifa kwako kukuambia, ‘Sisi tuko hapa’? Ni nani aliyeujalia moyo hekima au kuzipa akili ufahamu? Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu? Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni mavumbi yanapokuwa magumu, na mabonge ya udongo kushikamana pamoja? “Je, utamwindia simba jike mawindo, na kuwashibisha simba wenye njaa wakati wao wamejikunyata mapangoni mwao, au wakivizia kichakani? Ni nani ampaye kunguru chakula wakati makinda yake yanamlilia Mungu, yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula?